*Wafanyakazi wamwandikia Waziri waraka

*Waorodhesha majina 70 ya wanaowatuhumu

*Mkutano wa wafanyakazi waitishwa, waonywa

Wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji walioficha majina, wamemwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. John Nchimbi, waraka wakilalamikia vitendo vya ukabila ndani ya Idara hiyo. Katika waraka huo, wamedai kwamba karibu nafasi zote nono zimeshikwa na makabila mawili pekee yanayotoka Mkoa wa Kilimanjaro.

Madai kama haya ya makabila ya Mkoa wa Kilimanjaro kuhodhi nafasi kubwa yaliibuka miaka mitatu iliyopita ndani ya Jeshi la Polisi, ambalo kama ilivyo Uhamiaji, lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katika kuyapa nguvu madai yao, wameorodhesha majina 70 ya hao wanaodaiwa wanatoka Kilimanjaro, na ambao wamepangwa kwenye “vitengo vilivyonona”.


Wanaotajwa ni 1: Peniel Ombeni Mgonja 2: Isaack Bahati Fota 3: E. Crymont Nsowela 4:Dawson Emil Mongi 5: Nandula Patience Kombe 6: Anna Kyara Michael 7: Hannelore M Manyanga 8: Rogate Mingo Daniel 9: Joseph Henry Mtenga 10: Lusarago D Mreka 11: Gloria W. Mbasha 12: Peter William Lemery 13: Kale sylivia Joseph Utouh na 14: Violeth Kiwelu Eliabu.

 

Wengine ni 15: Felis Bilauri Mshana 16: Abdallah Musa Msangi 17: Liberatus Stanley Njuu 18: Mary Stella Majula 19: Joseph Francis Kasike 20: Sifael Stephen Tendwa 21: Novatus Aloyce Mlay 22: Beatrice Anamensa Kanza 23: Adinani Kidah Musa 24: Hendrick Fraita Mtu 25: Zakayo Leonard Lema 26: Novaita Edmund Mrosso 27: Moses Ismail Malisa 28: Dotto Roman Selasin 29: Christian Bernard Daat 30: Liberia Onesphony Manyanga 31: Christian Francis Mndeme 32: Frida Frant Maeda 33: Happiness William Kambuga 34. Triphonia Joseph Kinebo 35: Laurentia Isdom Blasius 36: Hilda Dawson Uiso 37: Tunu Mfinanga Asili 38: Marylen Msangeni Elisaria 39: Francis Noel Katawa 40: Irene Abel Mlack 41: Prosper Dions Mushi 42: Fasiruni Shabani Msofe 43: B Roman Kereti Pia kuna 44: Arnold Remy Mrema 45: Damian Roman Chikwa 46: Magreth Johnson Ngomuo 47: Hyasinter Ndewingla Tarimo 48: Salome Edgar Bolly 49: Gelard Honest Kawishe 50: Glory Ephraimu Mbuya 51: Hilgat Laurent Shauri 52: Paul John Mselle 53: Rose Robert Shayo 54: Patric Boniface Ngowi 55: Peter Jerome Kundy 56: Lucy Anselm Nyaki 57: Donald Lyimo Dustan 58: Siana Manasseh Kidin 59: Epiphania Joseph Lyimo 60: Juliana Selestine Mnerey 61: Lilian Humphrey Maleko 62: Raphael Timothy Maembe 63: Beatrice Elineema Lema 64: Lilian Emmanuel Lema 65: Irene Fraterine Lyamungu 66: Victor Stanley Ngowo 67: Jane Temu 68: Emmanuel Elihuruma Mrema 69: David Amani Minja 70: Ludovick Kavishe.

 

“Idara kwa sasa inaongozwa na Wachaga na kurithishana madaraka kwa ajili ya kulinda mtandao wao. Muasisi wa mtandao huu ni Kishe ambaye kwa sasa yupo Namanga kama mfawidhi. Huyu ndiye aliye mleta Mongi, Shayo, Kasike, Mtenga, Mgonja na kumuwekea mazingira ya kuwa mwanasheria wa Idara, Hannerole Manyanga.

 

“Hawa wamekamata utawala na kwa kupitia ofisi hiyo wameajiri na kuwapangia Wachaga na Wapare kwenye maeneo ya mikoa mikubwa ambako wanawasapoti kwa kuhakikisha wanapewa upendeleo katika nafasi za fedha hata kama hawana sifa hizo,” wamedai wafanyakazi hao.

 

“Mheshimiwa Nchimbi sisi hatuna ubaya na hawa watu na tunafanya kazi nao, lakini tabia zao zinatufanya tujiulize mustakabali wa Idara hii kwa vizazi vijavyo. Ebu angalia na hii ya hivi karibuni ambayo imetokea Tanga.

 

“Kuna afisa anaitwa Erasimus Francis ambaye naye ni Mchaga, alihamishwa kutoka Arusha kwenda Pangani kama adhabu baada ya uchakachuaji wa permit huko Arusha. Huyu afisa aliondoka kituoni kwake takriban miezi sita bila ruhusa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwake na Afisa Uhamiaji Mkoa DCI Nyaki (Mchaga) kama alivyowachukulia Afisa Gervas Mpangie wa Tanga, ambaye ni mgonjwa wa moyo na kutokana na maradhi yake ambayo ofisi inajua alienda matibabu na kuchelewa kurudi sasa ana jibu mashitaka; na kama alivyochukuliwa hatua Ghalib Yusuph wa Tanga ambaye alizidisha siku za likizo kwa sababu za kuuguliwa na wazazi, sasa anajibu mashitaka.

 

“Kwa huyu huyu hali ni tofauti. Hakuna barua toka kwa RIO Tanga. Lakini Honelole Manyanga, Joseph Francis Kasike na Mary stella( PHRO – Mpya na yeye Mchaga). Wamemtafuta na kumtaja Erasimus Francis kama msomi mzuri hivyo hawawezi kumpoteza na wamemhamisha kutoka Pangani hadi Chuoni Moshi (TRITA), na kumpeleka mafunzo.

 

Wanasema mtandao wao unaigharimu Idara. “Umebadili dhamira ya Afisa Uhamiaji kuwa ni mtumishi, badala yake Uhamiaji imekuwa ni kusaka fedha kwa njia zisizo halali.”

 

Wanadai kwamba Wachaga ni watumishi wa vituo vikubwa tu. “Huwezi kuwakuta Pemba ambako tunapelekwa siye tukionekana ni kero kwao.. Wana haki ya kutamba maana wamefanikiwa kukamata Idara ya Fedha- Peniel Mgonja, Joseph Mtenga -(Planning), Msaidizi wa Mhasibu Mkuu Jane Temu na Ludovick Kavishe – (system).

 

Wameikamata Idara. Permit yupo Dawson Mongi, Pasipoti yupo Hilgat L. Shauri. Sheria yupo Hannerole, Utumishi yupo Mary Stella na Joseph Kasike, Ununuzi yupo Mshana na Usafiri yupo Musa.

“Mtandao huu umetumika vibaya kwani hata baadhi ya maafisa uhamiaji mikoa wametumika kuuimarisha,” wamedai wafanyakazi hao kwenye waraka wao.

 

Wameongeza, “ Mheshimiwa Nchimbi, ukienda mikoani tembelea makao makuu ya mikoa na kituo chochote cha mpakani ambacho kipo active, utaona idadi ya Wachaga waliopo hapo na sehemu walizopangiwa…mtandao wao si mdogo, bali ni mkubwa na upo hata nje ya Idara na Wizara. Uteuzi ma- RIO wa hivi karibuni ni kero kabisa: Towo – Lindi, Kombe – Kagera, Rose – Njombe, Nyaki – Tanga, Mlay na Mosha – Tunduma, Kishe – Namanga, Masawe – Dodoma, RIO – Dar es Salaam. Sasa wamemsogeza Arnold Munuo kutoka Lusumo kuja Dar es Salaam kuja kuandaliwa kushika nafasi ya utumishi…

 

“Mheshimiwa Nchimbi hali hiyo ipo makao makuu tu, hao tuliowawekea vivuli ndiyo vinara wa mtandao huu katika vitengo mbalimbali. Mkakati tulio nalo ni kuanika uozo wote mikoani baada ya kukueleza ya Makao Makuu kwani hata huko mtandao umewaweka.”

 

JAMHURI imezungumza na Waziri Nchimbi, ambaye amesema hajausoma waraka huo, ingawa amepata taarifa za kuwapo kwake. “Nipo likizo, hao walioandika ni washamba kwa sababu awali tulipanga kuwa na kikao cha wafanyakazi wote, lakini kikaahirishwa. Pengine wameona watumie njia ya kuandika.

 

“Barua yao haina anuani, haina jina la mwandishi, huwezi kuijibu. Lakini Uhamiaji wajue kuwa wao ni Jeshi. Jeshini kuna utaratibu wa kuwasilisha malalamiko. Hatuwezi kutengeneza utaratibu wa kupokea taarifa za ‘anonymous’.

 

“Kwa kuwa nipo likizo sijui suala lao limefikia wapi, lakini naamini Naibu Waziri atakuwa amefuatilia. Jumatatu nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kulijua maana nitakuwa ofisini,” amesema Nchimbi.

 

Wakati Dk. Nchimbi akisema hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita wafanyakazi na viongozi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu, Dar es Salaam walikuwa na kikao cha pamoja.

 

Kamishna wa Utawala na Fedha, Peniel Mgonja, alitumia muda mrefu kuzungumza na wafanyakazi hao na kukemea vikali tabia ya kusambaza taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

 

Mgonja hakupatikana kueleza yaliyojiri kwenye mkutano huo, lakini chanzo chetu cha habari kilisema Kamishna huyo alisema kilichofanywa na baadhi ya watumishi hao ni kitu cha kitoto.

 

“Alisema si maadili ya Idara wala ya nchi ya kutoa tuhuma za aina hiyo katika vyombo vya habari.

“Akasema kama kweli kuna mtumishi anaona kuna jambo lisilo jema, anachoweza kufanya ni kushitaki kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi au akiamua anaweza kwenda Takukuru,” kilisema chanzo chetu.

 

Aidha, ilibainika kuwa walioshiriki kuandika waraka huo ni baadhi ya vijana, hasa kutokana na mambo hayo kuingizwa haraka haraka kwenye mitandao ya kijamii.

 

Kuna habari kwamba baadhi ya watumishi wana chuki kutokana na kutopandishwa vyeo na wengine kuondolewa kutokana na sababu mbalimbali, hasa udanganyifu na ukiukaji maadili.

 

“Kuna watumishi walioshushwa vyeo na wengine hawakupandishwa baada ya kubainika wamefanya ujanja ujanja-Katibu Mkuu akawarudishia vyeo vyao vya zamani. Hawa wamechukia kweli kweli.

 

“Lakini kuna wengine wamefukuzwa kutokana na tuhuma nzito, na ukiona namna walivyoandika majina yale matatu-matatu ya wanaowatuhumu, utaona kabisa kuwa hawa watu, ama wako ndani, au walikuwa ndani ya Idara,” kimesema chanzo chetu.

2717 Total Views 8 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!