Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF Julius Mtatiro anashikiliwa na Polisi katika kituo Kikuu cha Polisi tangu jana July 5, 2018.

Kwa muhibu wa alichoandika Zitto Kabwe katika Twitter yake na Facebook ni kuwa anahisi anatuhumiwa kwa kusambaza ujumbe uliomkashfu Rais Magufuli kupitia Facebook uliosema “Rais kitu gani bwana?”

Nanukuu alichoandika Zitto Kabwe “Juliaus  Mtatiro Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha CUF amekamatwa na polisi kwa kosa ambalo halijawekwa wazi Lakini linahusiana na ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii wenye maneno ‘ Rais Kitu gani Bwana ‘. Tutawajuza tupatapo Taarifa zaidi. Mshikamano mkubwa unahitajika kwa Kiongozi mwenzetu”

1711 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!