Updete Ajali ya Mv Nyerere Mwanza

RC wa Mwanza, John Mongela amesema idadi ya watu waliofariki kwa ajli ya kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 94 leo asubuhi. DC Ukerewe amesema Kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 na tani 25 za mizigo, lakini kibeba abiria zaidi ya 400.

 

Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio kuongeza kasi ya kuokoa na kuopoa watu waliopinduka na kivuko hicho. Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Simon Sirro na Waziri wa Uchukuzi Isaac Kamwelwe wamefika eneo la tukio kushiriki uokoaji.

 

Wakati uokoaji na uopoaji ukiendele mamia ya wakazi wa visiwa hivyo wamefurika kituo cha afya cha Bwisya kutambua jamaa zao walioopolewa. Tayari uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo   nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.