VIJANA 966 WAHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT

 Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa(Jkt)Kanal Hassan Mabena kulia akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kikosi cha 842 Kj Mlale jana wakati mkuu wa mkoa alipkwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali kwa vijana 966 Operesheni Mererani.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiangalia Tikiti maji katika Bustani ya kikosi cha 842 Kj Mlale JKT mkoani Ruvuma alipokwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo   ya vijana Operesheni Mererani jana.
 Mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt Luteni Kanali Absolomon Shausi akimuonesha  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma sehemu ya  Shamba la Mahindi  ya chakula yanayolimwa  na vijana  wa jeshi la kujenga Taifa katika kikosi hicho.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akitoa kitambaa kama Ishara ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la mradi wa ufugaji Kuku katika kikosi cha 842 Kj Mlale mkoani Ruvuma,anayemsaidia  kuondoa kitambaa ni mkuu wa kikosi  hicho    Lutewn Kanali Absolomon Shausi.
 Baadhi ya vijana wa  Jeshi la kujenga Taifa Operesheni Mererani 2018 waliopo katika kikosi cha 842 Kj Mlale wakionesha umahiri wa kuvuka vikwazo.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akikagua Gwaride maalum la vijana wa kujitolea waliomaliza mafunzo ya miezi minne ya kijeshi katika kikosi cha 842 Kj Mlale wilayani Songea ambapo jumla ya vijana 966 walimaliza mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi hicho.
 Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi cha 842 Kj Mlale Operesheni Mererani wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme(hayupo pichani)wakati wa kuhitimu mafunzo yao ya miezi minne katika kikosi hicho.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiongea na vijana,wazazi,Askari na maafisa mbalimbali wa jeshi la kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika kikosi cha 842 wakati wa kufunga mafunzo ya miezi minne ya kijeshi na Ujasiriamali kwa vijana 966 waliohitimu mafunzo yao jana,kushoto kwake ni mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Luten Kanal Absomlomon Shausi.