Baadhi ya Wachambuzi wa Soka nchini akiwemo kocha  wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo  amesema msa­nii wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza Ligi Kuu Bara, na kama aki­andaliwa vizuri anaweza kucheza hata Ulaya.

 

Julio ameyasema hayo akiwa kocha wa Team Sa­matta mara baada ya kum­alizika kwa mchezo maalum wa kuchangia elimu ulio­andaliwa na msanii huyo akishirikiana na Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya Genk nchini Ubelgiji. Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar, Team Samatta iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Team Kiba.

 

Julio alisema msanii huyo ni mchezaji mzuri na amekuwa akim­wambia kuwa yupo tayari kumsajili achezee katika timu yake kutokana na uwezo mkubwa alionao na kama akiwekwa vizuri ana uwezo wa kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

 

“Alikiba ni mchezaji mzuri sana, mimi binafsi huwa namwambia ‘nataka nikusa­jili’, kama hawezi kuja kule mkoani lakini tukija hapa Dar aje acheze, ana uwezo mkub­wa sana kuliko wachezaji wengi wa Simba na Yanga ambao wanalipwa mishahara ya bure.

“Isipokuwa tu nchi yetu haitaki kujua watu wenye uwezo, tunafua­ta majina na labda wana sababu zao, ndiyo hivyo lakini Kiba kama anatengenezwa hakuna ambaye anaweza kusema kuwa Kiba siyo mchezaji na kwa uwezo wake kama anacheza basi hapa ata­cheza ligi hii, mwaka wake mmoja tu anakwenda kucheza soka la kulipwa,” alisema Julio.

3415 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!