Na George Mganga

Klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii.

Yanga imezidi kujifua chini ya Kocha wake Mkuu, Mkongomani Mwinyi Zahera ambaye amekuwa mbogo kwa wachezaji wasio na nidhamu baada ya kuanza kuwaondoa kambini kila wanapochelewa kuripoti.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hussein Nyika, amesema kikosi kinapiga tizi la maana hivi sasa ili kuhakikisha kinapata ushindi dhidi ya walima alizeti hao kutoka Singida.
Nyika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili amewataka wanayanga wote kuhakikisha wanashikamana na kujitokeza kwa wingi uwanjani pale timu yao inapocheza ili kuwapa hamasa wachezaji wake.
Mabingwa hao mara 27 wa kihistoria katika ligi ya Tanzania wanaenda kucheza mechi hiyo bila presha wakiwa wameshinda mechi zao tatu mfululizo ikiwemo ya mwisho dhidi ya Stand United na kujikusanyia alama 9 kibindoni.
1394 Total Views 3 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!