JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Month: March 2020

Tukio hili tunalitafsirije? (1)

Nimeshtuka sana na kuingiwa wasiwasi kusikia eti yupo mbunge amediriki kuandika barua kwenda Benki ya Dunia kutaka zuio la fedha za maendeleo ya elimu hapa nchini. Nasema nimeshtuka kwa vile aliyetenda hivyo ninamfahamu kama ni askari wa Jeshi la Akiba…

Tumsaidie Rais kazi ngumu ya kuliongoza taifa

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliwahi kusema kuwa urais ni kazi ngumu, akaifananisha na mzigo mzito. Nayaamini maneno hayo ya mzee wa Kizanaki. Nimejitoa wazi kutaka kumsaidia rais wetu kupambana na ugumu huu ninaouona. Kwa sababu rais anaongoza…

Dhahabu, almasi nchini zaongezeka thamani

Thamani ya dhahabu na almasi zilizozalishwa nchini mwaka jana na kampuni kubwa zinazochimba madini hayo nchini iliongezeka kwa dola milioni 55.5 za Marekani ukilinganisha na kiasi kilichopatikana mwaka 2018. Kwa mujibu wa takwimu mpya za Benki Kuu ya Tanzania (BoT),…

IMF, AfDB wakosoa sera za uchumi Zimbabwe

Taasisi mbili kubwa za fedha duniani zimepinga sera ambazo Zimbabwe imeamua kuzitumia kufufua uchumi wake. Taasisi hizo, Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), zimesema Zimbabwe inahitaji kufanya mambo mengine mengi zaidi ya sera hizo iwapo…

Wataalamu wabaini chanzo cha nzige Afrika Mashariki

Wanaitwa nzige wa jangwani na mtu angeweza kuhisi kuwa wanastawi sana katika maeneo ya jangwani, lakini si hivyo. Nzige hawa ambao hivi sasa wanalitesa eneo la Afrika Mashariki wanastawi sana katika maeneo yenye mvua nyingi. Kwa miezi kadhaa sasa nchi…

Ndugu Rais, tumepakwa majivu usoni moyoni tumebadilika?

Ndugu Rais, Jumatano ya majivu zamani tuliita sikukuu ya majivu. Kumbe ndiyo mwanzo wa mfungo wa Kwaresma. Kabla ya Kristu waliofunga walivaa magunia. Badala ya kujipaka majivu usoni, walijimwagia mwili mzima. Kila walipopita walijulikana kuwa wamefunga. Wote walihesabiwa kuwa ni…