Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amepandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mapema Aprili, 2025.

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 baada ya kuitisha mageuzi ya uchaguzi na kuhimiza kususia uchaguzi ujao wa Oktoba.

Anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, ikiwa ni pamoja na madai kwamba alichochea uasi na kuwashutumu polisi kwa utovu wa nidhamu katika uchaguzi.

Awali mahakama ilijaribu kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao, lakini Lissu na timu yake ya wanasheria walipinga hili, wakitaja haja ya uwazi na taratibu zinazostahili.