Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kutangaza elimu ya ufugaji wa nyuki kwa sababu mwamko wa ufugaji huo bado uko chini.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya ufugaji
nyuki yaliyoandaliwa na TAMWA kwa ushirikiano na mfuko wa misitu
Tanzania, mkurugenzi mkuu Dkt. Rose Ruben amesema taasisi hiyo imedhamiria kujikita katika mradi wa ufugaji nyuki ili kuleta hamasa kwa jamii kufanya miradi hiyo kwa wingi.

Dkt. Rose amesema wanahabari wanachama walihudhuria mafunzo hayo ni vyema wakatumia kalamu zao kuwahamasisha wananchi wengine kufanya mradi huo kwa kuwa mwamko ni mdogo.

Amesema mradi huo utaanza kwa mizinga 200 ambapo utakuwa ukiendeshwa katika shamba la TAMWA liloko Kibaha, mkoani Pwani.

Amesema kwasababu ndiyo kwanza wameanza, wataendelea kuwatumia
wataalamu mbalimbali wa ufugaji nyuki kuwapatia mafunzo wanachama wao,
lengo la kuanzisha mradi huo litimie kama lilivyo pangwa.

Aidha, ameongeza kusema kwamba mradi huu, kwa kuwa ni wa kwanza kufanywa, tutakuwa na kipindi cha tathmini ili kuona kama wametimiza malengo, na pale ambapo wataona wamekosea, watarekebisha ili lengo
litimie.

“Tunaangalia wapi tumekosea, wapi tuweke juhudi zetu ili tutimize malengo hayo. Kama wanahabari, tutapeleka elimu hii kwa jamii kupitia karamu zetu ili jamii iweze kuona umuhimu wa zao” alisema.

Aidha, kwa wananchi ambao tayari wana maeneo yao ambayo hawajayaendeleza, yamekuwa mapori, wanaweza kutumia fursa hii kuweka miradi kama hii ya ufugaji nyuki, ambayo itawaletea pesa na kutunza mazingira ili kulinda mazingira na misitu yetu kwa ujumla isiharibiwe.

Mwezeshaji ambaye pia ni ofisa misitu wilayani Kibaha, Christina Samweli, amesema ufugaji wa nyuki ni muhimu sana kwa maendeleo ya sasa, hivyo ni vyema waandishi wakajikita katika eneo hilo ili kuleta hamasa. Amesema waandishi wana uwezo wa kutumia kalamu zao kukuza soko la ndani na la kimataifa.

Nashauri waandishi wa tamwa kuzingatia kwa makini umuhimu wa kuuza katika soko la kimataifa kwa kuhamasisha watu kuvuna mazao bora kwa kufuata mchakato unaozingatia viwango.

Amesema kuwa bidhaa zitakapokuwa na ubora, kama asali itakapovunwa ikiwa imekomaa, itakuwa rahisi kwa bidhaa zenu kufikia soko la kimataifa.

Hata hivyo, kama hatutafuata utaratibu mzuri wa uchakataji, tutapoteza soko la kimataifa.

Amedai kuwa kama wana tamwa, ni vyema kufanya kilimo cha ufugaji nyuki, kwani Tanzania bado haijafikia hatua nzuri katika soko la ufugaji nyuki.

“Tufuge nyuki kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa letu ili tuweze kujiinua kiuchumi pamoja na wanawake wa taifa letu.

Pia, nyuki wana faida katika kuchavusha mimea; asilimia 85 ya mimea duniani inachavushwa na nyuki, na asilimia 15 inachavushwa na vyanzo vingine kama maji na upepo.Hivyo, tukianzisha biashara ya ufugaji nyuki, pia tunahifadhi mazingira.

Amedai kuwa ufugaji wa nyuki utasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhifadhi mazingira.

xxxxxxxxxxx