Na Mwandishi Wetu, Doha, Qatar
Mkurugenzi Mtendaji na Daktari wa Norland Global Tanzania, Dkt Moses Makalla, amesema hapa kuwa amefurahishwa na mrejesho wa watumiaji wa dawa asili za kampuni yao hapa doha nchini Qatar.
“Ukimpa mgonjwa dawa au tiba lishe na akakurudushia mrejesho wa mafanikio, wewe daktari unafarijika sana. Hapa Qatar tunapokea mrejesho wa mafanikio kutoka kwa wateja wa magonjwa yasiyoambukiza ya muda mrefu. Tunafarijia sana. Dawa zetu zinazidi kung’ara Qatar,” ameeleza Dkt Malalla.
Amesema kampuni yao makao yake makuu yako China, lakini wagonjwa wa dawa zao siyo tu wako Tanzania na China bali hata Qatar ambako sasa hivi anasimamia matibabu na usambazaji wa dawa hizo. Ameeleza kuwa dawa zao zimepata umaafuru kwa sababu pia zinatumiwa kwa mafanikio na wanaanga wakiwa anga za juu.

Amesema kampuni ina ofisi zake katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha sasa hivi ipo Qatar. Norland Global Tanzania inajihisisha na utafiti, uzalishaji na usambazaji bidhaa za tiba mbadal.
“Hapa Qatar tunapata shuhuda za mafanikio ya watu waliotibika. Tunafarijika sana. Ni jambo zuri kwa pande zote mbili — sisi na wagonjwa wetu”, ameeleza Dk Makalla na kuongeza kuwa ingawa makao makuu yako China, kampuni ina mawakala katika nchi za Afrika.
Magonjwa anayosema yanatibwa na dawa zao ni pamoja na vidonda vya tumbo, presha ya kupanda na ya kushuka, changamoto za maaradhi ya macho, kinywa na meno, kansa;kurekebisha mfumo wa uzazi kwa wanawake na wanaume ili wapate watoto, maradhi ya viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu kama vile maradhi ya mgongo na miguu”, alisema Dk Makalla.
Kuhusu utafiti juu ya dawa zao, Dk Makalla ameeleza kuwa dawa zimefanyiwa utafiti wa kutosha na wataalamu wa kitaifa na kimataifa ili dawa ziwe na maana wakati wa sasa na zimeonekana hazina changamoto yoyote kwa binadamu zaidi ya kutibu magonjwa hasa yale yasiyo ya kuambukiza.

Lakini kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, aliseama, mwili wa binadamu umekuwa dhaifu kutokana na vifaa vinavyotumika katika maisha ya kila siku kama vile runinga, simu na kompyuta ambavyo huathiri macho. Viambata vingi vinavyotumika kutengenezea na kutunzia au kuhifadhia vyakula na vinywaji vinaathiri mwili kwa kiasi kikubwa.
“Matumizi ya hivyo vyote hufanya mwili wa binadamu kuwa na sumu nyingi mwilini ambayo hupelekea mwili kuwa dhaifu na kushambuliwa na maradhi mbalimbali. Tafiti zililenga yote haya, kwa hiyo dawa zetu zinalenga kuondoa sumu mwilini na kufanya mwili kuwa salama na kuongeza kinga ya mwili ili usishambuliwe na maradhi mbalimbali”, alisema Dk Makalla.
Amewaomba Watanzania kuchunguza afya zao mara kwa mara kutokana na mabadiliko yanayotokea duniani ili wapate matibabu mazuri mapema.