Na Aziza Nangwa, Dar es Salaam

Waandishi habari wametakiwa kusoma nyaraka mbalimbali za Sheria ya Tume huru ya Taifa na Sheria ya Uchaguzi Rais,Wabunge na Madiwani 2024 na marekebisho ya sheria ya vyama vya Siasa ili waweze kuandika habari zenye kuzingatia sheria na weledi kwa kulinda maslahi ya taifa letu.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu wakati wa mafunzo ya kuwanoa wanahabari ,kuhusu sheria ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 ambayo iliandaliwa na Media Brans kwa kushirikiana Taasisi ya Konrad Adenauer Stiftung –(KAS).

Jesse amesema mafunzo hayo yataweza kuwasadia waandishi wa habari kuripoti vizuri habari za uchaguzi mwaka huu ,kama watazitumia vizuri wataweza kuandika habari ambazo zitajenga mfumo mzuri wa kidemokrasi katikia nchi yetu na kukuza amani ya nchi yetu na kuongeza uwajibikaji
katika nchi yetu.

Amesema waandishi wanatakiwa kujua kwamba siasa ni maisha yanayomgusa
kila mmoja, hivyo hawawezi kuepuka cha msingi ni kuzingatia sheria zilizowekwa ili kulipoti habari zenye weledi ndani yake kwa sababu chaguzi ni hatua ya kwenda kuzitekeleza.

‘’Wanahabari lazima watambue kwamba uchaguzi ni mchakato na wanasiasa ndyo wanaobeba hatima ya kusimamia rasilimali zetu ,hivyo wanapaswa kuwahamasisha wananchi wakashiriki uchaguzi kwasababu ni
haki yao kuchagua viongozi sahihihi ambao wataongoza katika kipindi cha miaka mitano’’ amesema .

Amesema mafunzo hayo wameyatoa kwa Waandishi wa habari wa mkoa wa Dar
e salaam ni mahususi kwao kwasababu ya kujiandaa na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani lazima wazijue sheria mbilI mpya muhimu ambazo ni Sheria ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 na Sheria ya Rais,Wabunge , Madiwani 2024 sambamba na marekebisho ya sheria ya
vyama vya siasa ambapo zote mwaka huu kwenye uchaguzi mku zitatumika.

‘Kama tunavyofahamu kama waandishi wa habari wengi watakuwa bado hawajazipitia sheria hizo ,kwa hiyo tumejipa wajibu wa kutoa mafunzo kutokana na madhumuni ya kuwepo kwa kampuni yetu tumeamua kuwapa elimu kwa maana ya kuwaboreshea uwezo na maarifa yao juu ya sheria hizo ili ushiriki wao katika uchaguzi ulete tija katika nchi yetu

katika hayo vilevile tumeweza kuwajengea uwezo wa kuandika habari za jinsia kwa maana ya katika uchaguzi wanatakiwa kuchanganya jinsia, ili wanapo ripoti habari wazingatie haki ya kijinsia kwani takwimu za huko nyuma zinaonyesha habari hizo za kuchanganya jinsia wakati wa uchaguzi habari hizo hazikupewa kipaumbele ‘’amesema.

Amesema lengo la kampuni yao ni kushiriki katika tafiti za kihabarai mafunzo mbalimbali na kuazisha midahalo katika kujenga tasnia ya habari nchini kwa na kushirikiana na wadau mbalimbali pia kusukuma mbele tasnia ya habari kwa kuwajengea uwezo.

Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo Absalom Kibanda ,amesema kuwa kampuni yao tayari imeshafika katika mikoa saba kutoa elimu hiyo kwa waandishi mbalimbali ili waweze kuandika habari za uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Kibanda amesema lengo mafunzo katika mikoa hiyo ni kuwaanda waandishi wa habari kuzifahamu kwa undani sharia ambazo zinakwenda kusimamia uchaguzi mkuu mwaka huu ambapo kama wanahabari tunapaswa kuzijua ili kuepuka makosa ya kisheria.

Amesema wanahabari tunawakumbushana miiko na maadili ya uandishi katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu tukitambua na kuheshimu kwamba taasisi yenye dhamana iliyopewa majukumu ni hilo ni Tume huru
ya uchaguzi (INEC ).

‘Tunafanya hivyo tukijua kwamba taifa limeingia katika nyakati ambazo kumekuwa na udhibiti mkubwa Zaidi kupitia huduma za habari ambazo ni za 2016 ambayo kuna kanuni imetoa leseni za uandishi wa habari bodi ya ithibati ‘’amesema

Sisi tunachagiza hapo ili kuhakikisha wanao ripoti habari unazingatia weledi wa kitaaluma na kimaadili, huku tukiwalinda na majanga kwa kuepuka habari za uchochezi na potofu na kutambua katika kipindi hiki cha kidigitali kuna akili unde ili mwisho wa siku tuwasiwalishe Watanzania taarifa zisizo na usahihihi.