Kanisa la kihistoria ambalo limekuwepo kwa miaka 113 lililo hatarini kuzama kutokana na mtikiso wa chini ya ardhi linakaribia kuhamishwa lote jinsi lilivyo- kwa mwendo wa kilomita 5 (maili 3) kando ya barabara kaskazini mwa Uswidi.
Kanisa hilo lenye muundo wa mbao nyekundu huko Kiruna tangu 1912 umeinuliwa kwenye majukwaa makubwa kabla ya kuhamishwa katikati mwa jiji.
Litasafirishwa kwa kasi ya 500m kwa saa, na safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku mbili.
Kijiji cha kale kulipo kanisa hilo, kiko hatarini kutokana na ufa uliojitokeza ardhini baada ya zaidi ya karne ya uchimbaji wa madini ya chuma.
Hatua ya kuhamisha kanisa hilo ni moja ya matukio ya kuvutia zaidi na kipekee ya uhamishaji wa majengo makubwa huko Kiruna, ambayo iko kilomita 145 kaskazini mwa Mzingo wa Aktiki.
“Tumefanya matayarisho kabambe,” asema mtu anayesimamia uhamishaji huo, meneja wa mradi Stefan Holmblad Johansson.
“Ni tukio la kihistoria, operesheni kubwa sana na tata na hakuna sababu ya kutokea kwa makosa na kila kitu kiko chini ya udhibiti.”
Kufikia katikati ya miaka ya 2010, majengo mengine huko Kiruna tayari yalikuwa yakihamishwa hadi kwenye ardhi salama.
Mengi yalikuwa yamebomolewa na kujengwa upya, lakini baadhi ya majengo ya kihistoria yalihamishwa kama yalivyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka BBC
