Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema anaifahamu kwa kina mizigo ya Watanzania, ikiwemo changamoto za kilimo, ufugaji, biashara, uchimbaji madini, bodaboda na kusisitiza kuwa amedhamiria kuyatatua mara atakapochaguliwa.
Akizungumza na wananchi wa Katoro, Mkoani Geita leo Agosti 20, 2025 katika zoezi la udhamini, Mpina amesema nia yake ni kuingia Ikulu na kuunda Serikali yenye viongozi waaminifu, watakaoelekeza fedha za umma na rasilimali hizo katika kutatua matatizo ya wananchi.
“Taifa letu tupo kwenye wakati mgumu. Najua matatizo waliyonayo wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, bodaboda, mama ntilie, wachimbaji wadogo, machinga, na hata changamoto zingine mbalimbali Nimeamua kusimama kugombea ili kuyatatua matatizo haya,” amesema Mpina.




