Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Binti wa miaka 25 kutoka Kimara Baruti jijini Dar es Salaam, Jenipher Ayubu amefanikiwa shindia bidhaa kwenye minada mitatu yenye thamani ya zaidi ya Milioni kupitia jukwaa jipya la kidigitali la Piku.
Jukwaa la Piku limeanzishwa kwa lengo la kutoa fursa kwa wananchi kujikwapulia bidhaa za thamani kwa gharama nafuu kwanjia ya mnanda wakipeke ambapo dau dogo na la kipeke hushinda mnada huo.
Ayubu ambaye kwa muda mrefu alikuwa akitamani kumiliki saa za kifahari aina ya Coach pamoja na pafyumu yenye mvuto ya Jean Paul Gaultier Le Male Elixir sasa ndoto yake imetimia baada ya kuweka madau matatu madogo na la kipekee kwenye minada mitaty tofauti kupitia jukwaa hilo la Piku na hatimaye kujipatia bidhah hizo za kisasa.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi Ayubu amesema “Nilichotumia ni fedha ndogo tu, kitu cha ajabu ni kwamba sikuwa naamini kama kweli naweza kushinda. Lakini leo hii letewa bidha zangu bada ya jana usiku kupata ujumbe kuwa dau zangu zote tatu zimekuwa ndogo na zakipeke. Najivunia kuwa sehemu ya washindi wa Piku,” alisema Ayubu na kuongeza
“Ki ukweli sikuwahi kabisa kufikiria kujaribu kuingia katika jukwaa hili mpaka siku moja nilipoona tangazo la mshindi katika ukurasa wa Instagram wa Piku, niliona picha ya mshindi akiwa amekabidhiwa bidha zake na nikaamini jambo hili ni kweli hivyo pale pale nikashawishika kujaribu na leo nimekuwa mshindi ,” alisema kwa tabasamu pana huku akishikilia zawadi yake.
Ushindi huu si tu umemleta furaha kwa Ayubu bali pia umefungua ukurasa mpya wa matumaini kwake na kwa vijana wengine wengi wanaoamini kwamba kupitia teknolojia na ubunifu wa Kitanzania, kila kitu kinawezekana.
Piku ni jukwaa la kidigitali ambalo linamruhusu kila mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 mshiriki kushinda minada mbali mbali ndani ya jukwa hilo kwa kuweka dau la chini na kipeke lisilofikiriwa na mwingine. Mbinu hii ya kiubunifu inazidi kushika kasi miongoni mwa watu nchini, ikitoa matumaini mapya ya watu kumiliki bidhaa ambazo kwa kawaida zingehitaji gharama kubwa kumudu kununua.
Wabunifu wa Piku wamesema lengo lao ni kuwasaidia wananchi kwa ujumla kumiliki vifaa vya kisasa kama vile televisheni, simu janja, friji, ving’amuzi, manukati, magari na bidhaa nyinginezo ilikutimiza ndoto zao. “Tunataka kila Mtanzania ajisikiye kuwa ana nafasi ya kumiliki bidhaa anazozihitaji, bila kujali kipato chake,” alisema Barnabas Mbunda ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Piku.
