Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia,
Dar es Salaam

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Wakulima (AAFP), Mark Isdory Mhemela ameipongeza Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) kwa kusimamia vizuri zoezi la uteuzi wa wagombea kuanzia ngazi ya Urais,Ubunge na Udiwani.

Akizungumza kwa njia ya simu mapema asubuhi Agosti 29,2025 amesema kwamba yeye mgombea wa nafasi ya ubunge ,ameona jinsi INEC walivyofanikisha zoezi hilo kwa ufanisi kwani wagombea wote wameteuliwa bila tatizo lolote.

“Naipongeza Serikali kupitia Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwapatia usafiri wagombea wa nafasi ya Urais ,hii ni mara ya kwanza kwa kujali”,amesema Mhemela

Aidha,amesema kwamba anatarajiwa kuanza kampeni Septemba 5,2025 katika Jimbo la Mtumba Jijini Dodoma,hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi kupitia chama chake.

Pia, amewataka vijana,wazee na wanawake wenye mapenzi mema na AAFP kwa kushiriki kwa wingi katika Uzinduzi huo wa kampeni kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi hivyo naomba waniunge mkono.

“Niwaombe vijana wenzangu wajitokeze kwa wingi waendesha bodaboda,bajaji na wote ambao wanatafuta ajira kuja kushiriki kampeni pamoja na wazee na wanawake wote kwa ajili kusikiliza sera na Ilani za Chama”,amesema Mhemela.