Monalisa Joseph Ndala, mwanachama wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, leo 03 Septemba 2025, amewasilisha malalamiko rasmi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nikiiomba ichukue hatua kali na za kinidhamu kwa haraka dhidi ya chama changu kutokana na mwenendo wake wa mara kwa mara wa kuvunja Katiba ya chama na Sheria ya Vyama vya Siasa Sura 258.

Kwa mujibu wa taarifa aliyotuma kwenye vyombo vya habaru, amesema amefikia uamuzi huo kutokana na ukweli kwamba katika muda mchache yaani  chini ya mwezi mmoja chama kupitia uongozi kimeshiriki kufanya uvunjifu huo kwa;-Kukiuka Utaratibu wa Kikatiba na Kisheria;

Chama kimehusika katika mchakato wa kumuingiza na kumteua Bw. Luhaga Mpina bila kufuata utaratibu wa kikatiba na kanuni za chama. Uteuzi huo umefanyika kinyume na taratibu zinazotambulika na zinazolindwa na sheria ya usajili wa vyama vya siasa.

Kitendo batili cha kuvuliwa uanachama Mnamo tarehe 28 Agosti 2025, Tawi la Mafifi – Iringa Mjini kilitoa barua ya Kumb. Na. ACT/IR/IRM/KH/MF/001 kikieleza kwamba amepoteza sifa za kuwa mwanachama. Kitendo hiki ni uvunjifu wa Katiba ya chama na Sheria ya Vyama vya Siasa kwa sababu:

    Kwa kuzingatia ukiukwaji huu wa kikatiba na kisheria, anaiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa; Ichukue hatua kali na za kinidhamu mara moja dhidi ya chama cha ACT Wazalendo kwa kuvunja Katiba na Sheria ya Usajili wa Vyama vya Siasa.

    Kufuta uamuzi batili uliotolewa na Tawi la Mafifi – Iringa Mjini dhidi yake; amekielekeza chama kuhakikisha taratibu, sheria na katiba vinazingatiwa ipasavyo katika masuala ya uteuzi wa viongozi na usimamizi wa wanachama.