
Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewahimiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi Vitongoji, Vijiji na Kata kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 10, 2025 katika Kata ya Ng’anzo wilayani Bukombe ambapo amesema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili kura zote za Ndiyo ili aweze kuongoza nchi kwa kipindi kingine na kukamilisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya maji, umeme na miundombinu.
“ Viongozi hamasisheni wananchi tarehe 29 Oktoba wamchague Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ametuletea maendeleo na kwa kumchagua yeye tutaendelea kupata maendeleo mengine mengi. Nawaomba pia mnichague mimi Dkt. Doto Biteko ili tukamilishe yale tuliyokwisha yaanzisha lakini pia mtuchagulie Diwani wa CCM, Ndugu Mashaka na kuchagua viongozi wa CCM ni kuchagua maendeleo ya nchi hii”


