Na Mwandishi, JamhuriMedia, Tabora
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Nkumba, amesema mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kwa kupeleka sh trilioni 6.42 katika kuchagiza maendeleo mkoani humo.
Amesema fedha hizo imegharamia miradi mbalimbali na kupunguza changamoto zilizokuwapo na kuleta fursa kubwa kwa wananchi.
Amesema wana kazi kubwa ya kwenda kwa wananchi kueleza sera za chama hicho ili waelewe na mwisho wa siku wakipigie kura Oktoba 29.
Amesema kuna baadhi ya wenzao wameanza kwenda kwa wananchi kuzungumza suala la mchakato wa uchaguzi.
“Tumebana kila kona tunakwenda kwa wananchi, tuna uhakika wananchi hawa watafanya jambo kubwa Oktoba 29, mwaka huu.
‘Twendeni tukampe kura za heshima na kishindo, tupo vizuri, isifike mahali tukabweteka eti sehemu fulani hakuna wapinzani.
