Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Media, Buhigwe
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema ataboresha sekta ya kilimo kupitia zao tangawizi.
Akihutubia mkutano wa kampeni wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo Septemba 13,2025, Samia amesema serikali imepanga kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya tangawizi ili kuhakikisha wakulima wananufaika zaidi na zao hilo.
Amesema ubunifu na viwanda vya kuchakata mazao ni sehemu muhimu ya ajenda ya kuinua uchumi wa wakulima kwa wananchi.
Amesema juhudi sawia zinaenda na miradi mingine ya maendeleo kama vile ujenzi wa barabara, umeme kutoka mradi wa Malagarasi (megawati 46), na miradi ya maji vijijini, ambayo yote inalenga kuimarisha mazingira ya uzalishaji.

