*Mikataba ujenzi wa kiwanda cha meli waanza
*Umeme wafika vijiji vyote, SGR kupaisha uchumi
*Ujenzi wa barabara lami kubaki historia
*Fidia ujenzi uwanja wa ndege kulipwa haraka

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kigoma

Mgombe urasi wa Chama cha Mapinduzi Samia Suluhu Hassan amesema ahadi zake zote anazitoa kwa wananchi atazifanya kazi na hakuna kitakochosimama.


Samia ametoa kauli hii wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Kigoma wakati wa mkutano wa mwisho wa kampeni mkoani humo mwishoni mwa wiki, huku akisisitiza ilani mambo mengi yamefanyika yataendelea kusimamiwa ipasavyo.


Ni imani yangu kwamba tumetimiza ahadi zetu kwa wanannchi, miongoni mwa ahadi za CCM na serikali yake ambazo waliweka kwa wana Kigoma ilikuwa kuutoa mkoa wa Kigoma kwenye mkoa wa pombezoni na kuufanya mkoa wa kimkakati, hili ni dhahiri sasa linaonekana.


si mkoa tena wa pembeni bali mkoa wa kimkatati na siyo mwisho wa reli bali ni kitovu cha biashara na maendeleo, kwa uwezo wa Mungu tutakamamilisha,amesema.


Amesema ili kufikia lengo hilo, kwenye miundombini ya usafiri na usafirishaji ambao ndiyo mhimili mkubwa wamejidhatiti kuunganisha mkoa huo kwa njia zote za anga, barabara, anga na njia ya maji.


Tayari maboresho ya uwanja wa ndege kama ilivyosema hapa yanaendelea na njia imeanza kutumia, mradi huu ni sehemu ya mpango mpana wa kitaifa kwa kulifungua anga la Tanzania na kuliimaeisha shirika letu la ndege ambalo ndege zake zinatua hapa.

Shirika letu limezidi kupanua mabawa yake na hivi karibuni linatarajiwa kuanzisha safari za ndege kwenda Lagos, Nigeria kwa sasa tunafanya maboresho ya viwanja vya 14 ndania ya Tanzania ambako sita vimekamilika na vinane tunaendelea na ukamilishaji wake.


Amesema kwenye sekta ya reli ya kisasa Kigoma ni sehemu muhimu mno kwenye reli ya SGR kwa sababu kuna vipande viwili kuanzia kipande cha sita Tabora- Kigoma na kipande cha saba cha Uvinza Msongati.


Baada ya kufika hapa kigoma, reli hii itakwenda Burundi na hatimaye mashiriki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mmeona tumekamilisha sehemu ya kwanza na ya pili ya Dar es Salaam hadi Dodoma na sehemu zote kwa maana ya sehemu ya tatu, nne na tano ambayo ni Mwanza-Isaka tutaikamilisha mwaka huu ya sita ni Tabora-Kigoma na Uvinza- Msongati kazi inaendelea,amesema.


Amesema sambamba na hili anaendelea na maboresho ya reli iliyopo ambayo ni ya zamani (MGR) kwani vichwa vitatu vya treni vimenunuliwa, mabehewa mapya 22 ya abiria na ya mizigo 44.


Vilevile tumeleta mabehwa 350 ya mizigo na 33 ya abiria, sasa navyosema tunayafanyia ukarabati na mengi yao tayari yamekwisha kamilika, kazi hii tumeifanya kwa kushirikiana na wabia wetu ambao wamekarabati mabehwa 60 pamoja na mengine 8 yanayotunza ubaridi kwa ajili ya kusafirisha mazao ya matunda na mbogamboga.


Tumefanya maboresho ya kanuni kuhusu uendeshaji wa huduma ndani ya reli na sasa kanuni na sheria zinaruhusu waendeshaji binafsi kufanya biashara kwenye miuondombinu ya reli iliyotandikwa na serikali ya Jamhuri ya ya Muungano wa Tanzania.


Kwa hiyo mambo ya uendeshaji tutafanya sisi serikali na watu binafsi ambao tutaona wanaweza kwendana na sisi ili kuleta ufanisi wa usafirishaji wa uendeshaji wa mizigo na abiria ili uchumi wetu ukuwe haraka,amesema.


Kwa upande wa usafiri wa majini, Samia amesema wametekeleza miradi mikubwa kwenye maziwa makuu ikiwamo ujenzi na ukarabati wa meli za abiria na mizigo.


Kwa upande wa Ziwa Tanganyika hasa mkoa wa Kigoma, serikali inaendele ujenzi wa bandari za Ujiji, Kibirizi na Kabwe na bandari ya Kalema na Kasanga ziliko mkoani Rukwa.Pia tunajenga meli nne kwenye bandari ya Kalema ambako moja imekalimika na nyingine tatu ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Matarajio ni kwamba meli hizi zikikamilika zitahudumia Tanzania pamoja na nchi jirani za DRC, Burundi, na Zambia,amesema.
Amesema mwaka jana, serikali ilianza kazi ya ukarabati wa meli kongwe ikiwamo ya MV Liemba ambao unatarajia kukamilisha mwaka ujao wa fedha.


Tunapokwenda mbele mkitupa ridhaa yenu tutakuwa na mradi mwingine mkubwa wa kuunganisha reli na usafiri wa meli.

Tayari tumesaini mikataba mitatu ya ujenzi wa kiwanda cha meli ambao umeanza kutekelezwa eneo la Katabe, ujenzi wa meli wa mbili za mizigo na moja kwa ajili ya Ziwa Tanganyika na nyingine kwa ajili ya Ziwa Victoria.


Meli ya Ziwa Tanganyika itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3,500 itakayokuwa na ghorofa mbli (juu na chini). Meli hizi maalumu zitapokea shehena ya mizigo zinazosafirisha na reli ya SGR kutoka bandari za bahari ya Hindi yaani bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara kama kuna mizigo kule kwa sababu Mtwara tumeiweka kwa sababu maalumu kwa ajili ya masuala ya pembejeo za kilimo na mambo mengine, zitashushwa Dar es Salaam kisha kwenda maeneo mengine,amesema.


Amesema miradi ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa majini inaendelezwa kote nchini ikiwamo Bandari ya Hindi na Ziwa Victoria, Nyasa na Victoria.


Leo nimetaka kujikita zaidi kwenye miradi ya Ziwa Tanganyika husasan hapa Kigoma. Miundombinu ya barabara ndugu zangu tumefanya jitihada kubwa na kuhakikisha miradi yote ya barabara inakamilika ikiwamo vipande vyote vilivyo salia vya barabara kubwa inayotoka Manyovu hadi mpakani pamoja na zingine nilizoahidi katika mikutano yangu ya Buhigwe, Uvinza na Kasulu,amesema.


Amesema ahadi nyingine ni kuhakikisha barabara zote za vijijini ambazo haziko kwenye mpango wa kujengwa kwa lami zinajengwa kwa changarawe na kufanya zipitike msimu yote mwaka mzima.


Kwa upande wa umeme yamesema mengi hapa, lakini tunatekeleza mradi wa Malagarasi ambao utazalisha megawati 50, tutajenga msongo wa KV 132 kutoka Malagarasi hadi KIdahwe wenye urefu wa kilomita 54 ambao utaweka umeme pale na kituo kitapokea na kupoza kisha kusambaza.


Pamoja na kufanya hayo hapa Kigoma, tumefikisha miundomboni ya umeme kwenye vijiji vyote, sasa tunamalizia vitongoji ndani ya mkoa huu,amesema.


Kuhusu fidia, amesema kama kuna maeneo ya wananchi yamechukuliwa atahakikisha fidia zao zinalipwa kwa sababu wanafanya uchambuzi na uhakiki na zile ambazo zitatambulika thamani yake zitalipwa.


Serikali ya CCM haidhurumu mtu, tutakuja kuzilipa fidia zote. Uwapo wa umeme wa kutosha ndani ya Kigoma utavuta na kujenga mazingira ya uwekezaji ndani ya mkoa huu.

Kwa mfano kule Kasulu tayari uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha sukari (Kasulu Sugar). Kiwanda hiki tayari kimeajiri watu 500, kikianza kufanya kazi yake kikamilifu kitaongeza sukari nchini na kuleta utulivu wa bei ya walaji wa sukari, pia kuna kiwanda cha saruji ambacho kinazalisha saruji sasa kwenye soko la mkoa na nchi jirani, tuna mpengo wa kuleta viwanda vingi,amesema.


Amesema kamwe hawezi kusahau suala la kongani za viwanda kwa vijana kuongeza thamani kwa mazao yanayozaliwa katika wilaya tofauti.


Pamoja na saluji na sukari, taifa letu tumejipanga kuhakikisha tunajitosheleza kwenye mafuta ya kupikia au ya kula na michikichi ni sehemu ya mpango huo.Nafahamu bado kuna eneo la kulima chikichi bado halijafanyiwa kazi, uhitaji wa miche karibu milioni moja bado halijafanyiwa kazi.

Sasa niwaombe ndugu zangu wakulima wa michikichi ndani ya mkoa, serikali mkitupa ridhaa tunakwenda kujielekeza kwenye eneo kwa nguvu kubwa ili tupate mali ghafi nyingi tuvutie kiwanda cha kuchakata chikichi na kutengeneza mafuta hapa nchini,amesema.


Amesema atatoa ruzuku ya miche na mambo mengi yote ya msingi ambayo yanahitaji ili zao hilo lilimwe kwa wingi.


Amesema serikali ina mkakati wa kuona wawekezaji wengi zaidi wanamiminika mkoani humo uzuri wa Kigoma ni kwamba soko lipo hapa jirani kila kinachozalishwa kikivuka kwenda Burundi na DRC hayo ni masoko yetu makubwa na wala hatuwezi kukamilisha mahitaji yao, naowamba wana Kigoma tujielekeze huku na uzuri ni kwamba nimeona vibendera vya Burundi kwenye nyumba fulani Fulani hapa mjini, hii inaonyesha hawa ndugu wamefungua balozi, lakini na ofisi kadhaa za kuhamasisha na kuratibu ufanyaji wa biashara baina yetu na wao,amesema.


Amesema ahadi kubwa kila kwa wanancho wa mkoa huo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma safi za afya, elimu, kuanzia chekechea hadi hadi chuo kikuu, kuhakikisha mkoa una ngaa umeme vitongoji vyote, kila mwananchi kupata maji safi na salama.


Amewahakikisha wafugaji ni kuendeleza ujenzi wa majosho, mabwawa, chanjo kwa ajili ya afya ya mifugo, kuboresha machinjio.
Amesema kwa upande wa uvuvi wameanza kupeleka boti ambako kwa sasa kuna vizimba 26 na boti mbili za uvuvi.


Mkitupatia ridhaa ya kuongoza tena tutaongeza boti na vizimba ili wavuvi wazidi kuvua samaki wengi na kuwapeleka sokoni.

Tutaendelea kuwazesha wafanyabiashara na vijana kupitia mikopo ya vikundi mbalimbali kama mlivyokisikia wakati nikizundua kampeni nilisema tutatenga shilingi bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara ndogo ndogo, tumejipnga kutimiza vipanda vya machinga pale Kibilizi, kazi hii tumewapa wizara ya Uchukuzi wanapoendeleza na kuboresha bandari ya kigoma basi wafanye na hili pia. Mamlaka ya Bandari ndiyo jukumu la kuboresha mazingira haya,amesema