Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam

Mgombea udiwani Kata ya Tandika Uzairu Abdul Athumani kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM amewaahindi wananchi endapo watampatia ridhaa ya kumpa kura za kishindo Oktoba 29,2025 atahakikisha anatatua kero zinazowakabili ikiwemo michango sumbufu kwa wanafunzi shuleni na tozo za leseni za wafanyabiashara TRA

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni jana Dar es Salaam amebainisha kuwa kero hiyo ya michango kwa wanafunzi shuleni bila kushirikisha wadau ambao ndiyo wazazi anakwenda kulifanyia kazi ndani ya siku 100 atakapoingia madarakani.

“Suala hili la michango shuleni limenifikia ni kero ambayo imefikia hatua mwalimu anadamka na fimbo asubuhi na mapema anakaa Mlangoni kukusanya fedha kwa wanafunzi aliyekuwa nayo bila kuangalia anaadhibiwa ambapo yeye hana kosa bali mzazi kiukweli kuna Shule nilikwenda nikaikuta hii Hali niliumia sanaa” amesema Uzairu.

Sambamba na hayo amebainisha kuwa CCM imefanya mambo makubwa kwenye kata ya Tandika,ikiwemo afya ya hapo awali suala walikuwa wanafuta huduma mbali lakini kwa sasa wanatembea kwa kilometa chache kufuta huduma i ambapo Dkt Samia Suluhu Hassan mgombea nafasi ya urahisi kwa tiketi ya CCM kwa kushirikia na viongozi wake huduma zimesogezwa Karibu na Wananchi amejali afya za wana Tandika,naye Mpeni Kura

Aidha alihaidi ndani ya miaka mitano ijayo kituo cha Afya cha Tandika kitafanya kazi kwa masaa 24 tofauti na sasa kikifanya kazi kwa masaa 12,hilo linawezekana sababu njia sahihi ni kuongeza rasilimali watu na hilo litafanyika,lakini eneo la kujifungulia wakinamama linafanya kazi kwa masaa 24.

Awali mbunge Mstaafu Dorothy Kilave akimwombea kura Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ,Mbunge wa Temeke Masiam Kisangi, na diwani Uzairu Athumani amesema CCM ni Chama makini kina watu makini hivyo Oktoba 29 mwaka huu mwananchi asifanye makosa.