Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania(JWT) Mkoa wa Dodoma imepongeza jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na uongozi wake kwa kazi nzuri katika kuhakikisha nchi inakua kwa utulivu na amani hali inayorahisisha biashara na uwekezaji kuendelea kufanyika bila vikwazo.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Alexander Mallya,amezungumza hayo leo Sept 17,2025 Jijini hapa katika mkutano wa mrejesho wa wafanyabiashara ambapo amesema kuwa makusanyo ya kodi mkoani Dodoma yamefikia bilioni 204, ukiwa umezidi lengo la awali la bilioni 88.

“Tunapolipa kodi ndipo tunachojenga majengo ya kijamii, barabara, viwanja vya ndege, na miradi mikubwa ya maendeleo,” amesema Mallya.

Akizungumza na waandiashi wa habari amesema kuimarika kwa ukusanyaji mapato kunatokana na Wafanyabiashara kumenufaika moja kwa moja na maendeleo kama Mji wa Magufuli City, mradi wa SGR unaowezesha usafirishaji wa mizigo kwa urahisi, na msalato wa ndege unaotarajiwa kuwa kimataifa.

Aidha amesema barabara za mkoa wa Dodoma zikiwa zinaendelea kufanyiwa maboresho wao kama wadau wakubwa wana matumaini kuwa zitarahisisha usafirishaji wa bidhaa na biashara na kuondoa vikwazo vyote vya usafiri.

Mallya amebainisha kuwa jumla ya kero 118 zilizokuwa zinashughulikiwa zimepungua hadi 18 pekee, huku kero 36 zikiwa bado zinafanyiwa utatuzi.

Ametaja Miongoni mwa kero zilizokamilika ni punguzo la VAT, msongamano wa huduma bandarini, na matatizo ya kero za wakulima huku akisisitiza kuwa kuunganisha kodi zote katika “kapu moja” kutarahisisha malipo na kupunguza urasimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma, Gilbert Chuwa, amesisitiza kuwa kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi na kuwahimiza kuwa kila mfanyabiashara ana wajibu wa kulipa kodi na kusisitiza kuwa Serikali haijawahi na wala haiwezi kumtoza MTU kodi bila kuzingatia hali ya biashara .

“Tuendelee kuhamasishana kulipa kodi,kwa kufanya hivyo, tunahakikisha miradi mikubwa inafanikishwa, wafanyabiashara wadogo wanasaidiwa, na mji wetu unakua kwa kasi,” amesema Chuwa.

Amesisitiza kuwa Serikali inapaswa kutoa elimu kwa wafanyabiashara wapya ili kuibua fursa zaidi za uwekezaji.

Baadhi ya Wafanyabiashara wa Dodoma wanawaomba Watanzania kuendelea kumchagua Rais Samia katika uchaguzi ujao ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanaendelea kwa tija na maendeleo ya nchi.

Sylivano James Chami amesema, “
Serikali chini ya Rais Samia imefanya kazi kubwa, wafanyabiashara sasa tunafanya biashara kwa urahisi bila kuogopa kufungwa kwa maduka kwa sababu za madeni,” amesema