Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Zanzibar

Mgombea ubunge Jimbo la Makunduchi, Wanu Hafidh Ameir (CCM), amesema anajivunia umoja na mshikamano wa amani na umoja uliopo.


Wanu ametoa kauli hiyo leo Septamba 17,2025 alipopewa nafasi ya kusalimia maelfu ya wafuasi wa CCM katika mkutano wa kampeni katika Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.


Amesema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mgombea urais wa Zanzibar, Dk Ali Hassan Mwinyi, wamefanya kazi kubwa na kuendeleza amani, umoja na mshikamo vitu ambayo vimeendelea kutawala mpaka sasa.


amesema kumekuwa na mapinduzi makubwa katika sekta tofauti kama vile uchumi wa Bluu ambao umefanywa na kusimamiwa na Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi.


Amesema kumekuwapo ongezeko kubwa la ajira kwa vijana kutokana na uwapo wa fursa nyingi za ajira.


Pia amesema viongozi hao, wamejenga shule mbalimbali za msingi na Sekondari kutokana na fedha za covid hivyo kupunguza kabisa tatizo la watoto kupata nafasi za kusoma.


Amesema katika miaka mitano iliyopita, wamewezesha shule za Mkoa wa Kusini Unguja kuingia kwenye 10 katika mitihani ya Taifa.


” Wana Kusini mtatoa kura, inueni mikono nione, wataweza kweli,”amesema.
“Wana Makunduchi wameniambia kura zipo za kutosha kwako mwenyekiti wetu pamoja na Dk Mwinyi.