Mgombea Urais kupitia cha cha wakulima AAFP Kunje Ngombalemwilu amesema pindi atakapopata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha anajenga madarasa kwa ajili ya kufundisha uzalendo na maadili ambapo elimu hiyo itatolewa na wastaafu nchini.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kampeni zake anazoendelea nazo nchini kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 29,2025.

Amesema nchi inashindwa kuendelea kwa sababu haina uzalendo na kuheshimiana hali iliyopelekea watu kufanyakazi kwa mazoe bila kujali maslahi ya nchi na wananchi wake.
“Hii inchi imekosa maheshimiano na uzalendo serikali yangu itahaikisha hii hali inakoma watu watafanyakazi kwa maslahi ya Taifa lakini wala rushwa nitawashughulikia watakula viboko na nitatengeneza bwawa la mamba ikulu ili watakaobainika wamekula rushwa watadumbukizwa na kuliwa na mamba”,Amesema.
Ameongeza kuwa serikali yake itahakikisha ulinzi mipakani unaimalika kwa kutoruhusu watu kutoka mataifa mengine kuingia nchini kwani ametaja watu hao kuwa sehemu ya mmomonyoko wa maadili uliopo nchini.
“Hii inchi vijana wamekuwa na tabia za ovyo kwa sababu ya kuruhusu mataifa mengine kuingia na kuleta tabia zao sasa niwaambie kabisa watoto wakiume mnaovaa heleni kwenye masikio yenu hasa wasanii nitakuwa ninawachapa viboko 12 kwani serikali yangu itazingatia zaidi maadili na uzalendo”,Amesema.
Akizungumzia mchakato wa upatikanaji katiba mpya amesema serikali yake haitashughulikia swala la katiba kwa haraka badala yake ataendelea na katiba iliyopo katika kipindi chote cha miaka mitano ili kuwaenzi waasisi wa nchi ambao waliandaa katiba hiyo.

“Niwaambie wananchi serikali yangu haitashughulikia swala la katiba mpya nitatumia iliyopo ili kuwaenzi waasisi huku nikijenga madarasa maalumu kwa ajili ya kuwafundishia na kuwaelimisha wanachi kuhusu katiba kwa kuwapatia katiba iliyopo na katiba iliyopendekezwa ili wao ndio waseme wanataka katiba ya namna gani”,Amesema
Amesema kama hakuna uzalendo basi katiba haitafanya kazi yeyote hivyo atahakikisha uzalendo unapatikana kwanza ndio katiba ifuate kwani ameitaja katiba hiyo kama roho ya wananchi.
Nae Mgombea Mwenza Chumu Abdallah amewataka wananchi kuhakikisha wanakichagua chama hicho kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ya kweli na mabadiliko ambayo yatakuwa na manufaa kwa wananchi.

