Na Mwandishi wetu, Jamhuri Media, Pemba
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mratibu wa Kampeni Kanda ya Pemba, Mohamed Aboud amesema Watanzania wa pande zote mbili sasa wanaishi kwa amani na mshikamno mkubwa.
Amesema hayo Septemba 20,2025 alipopewa nafasi ya kusamilia na kutoa neno katika mkutano mkubwa wa kampeniza Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani Pemba.

Amesema wamejipanga kupiga kura kwa wagombea wote kuanzia ngazi ya diwani hadi rais ili kujenga safu imara itakayosaidia kusongeza na kupeleka mbele maendeleo.
Sasa kuna marafiki zangu ganda la mua wameona kivuno, hawakujua ndani ya CCM tuna utaratibu wa kutafuta wagombea na tukishapata wagombea wale waliojitokeza tunaunga pamoja, sasa hiyo kwa pamoja hiyo tabia yao ya kuokota wajue tulikuwa naye marehemu Edward Lowassa wakamkimbilia akarudi nyumbani, tulikuwa naye rafiki ndugu Membe (Bernard) naye mwenyezi Mungu ampumzishe, wakamkimbilia akarudi nyumbani, sasa wasije kulalamika kwa huyo waliyemfuata wakamkumbatia wajue ni ganda la mua la jana, chungu kanaona nini!Oktoba tunatiki.

