Na Kulwa Karedia, Jamhuri Media-Nyasa
Mgombea urais wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amasema serikali itajenga reli ya kisasa yenye urefu wa kilomita 1,000 kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Samia ametoa kauli hiyo septemba 21, 2025 wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Nyasa wakati mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu mkoani Ruvuma.
Amesema lengo kubwa la ujenzi wa reli hiyo ni kuunganisha maeneo maalumu na ya kimkakati, hasa ya kilimo na eneo la Liganga na Mchuchuma ambako kuna uzalishaji mkubwa wa makaa ya mawe.

Tumekaa na aliyesema anatengeneza kuna mambo alisema turekebishe tumefanya hivyo na sasa tuko kwenye mazungumzo mengine, mradi huu ni reli ya kilomita 10000 ambayo itapita maeneo yenye utajiri mkubwa wa mazao ya nafaka na kuunganisha maeneo ya Liganga na Mchuchuma yenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe.
Tuko kwenye mazungumzo tuje kujenga reli hii ya kisasa kwa kiwango cha kisasa kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay, haya ndiyo tunayoyafikiria kwa wilaya ya Nyasa. Ni wazi reli hii tukiweza kuijenga itaambatana na manufaa makubwa sana kwa ukanda wa kusini, sasa niwaulize nani kama CCM. Tuna miradi mikubwa mitatu, mosi bandari zetu mbili, barabara inayounganisha hizi bandari na reli,amesema.
Amesema Septemba mwaka jana alifika wilayani Nyasa ikiwa ni sehemu ya ziara ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ya wananchi ambako alikagua na kuzindua miradi mbalimbali.

Amesema ziara hiyo ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ambayo kwa uwezo wa uwezo wa Mungu wameitekeleza kwa mafanikio makubwa.
Ndiyo sababu tunmekuwa na ujasiri mkubwa wa kurudi tena kwenu na kuinadi ilani mpya ya mwaka 2025-2030 kweny ndugu wananchi itakayokwenda kutekeleza mambo kadhaa ambayo itakayoleta maendeleo na kustawisha hali za wananchi mambo makubwa zaidi.
Nilipokuja Sepetmba hapa, niliweka jiwe la ujenzi wa Bandari ya Bambay Bay, ninayo furaka utekelezaji wake umeanza na unaendelea vizuri na ile ndoto ya muda mrefu ya wana Nyasa au wana Mbambay Bay kuwa na bandari ya uhakika inaelekea kutimia mapema mwakani.

Vilevile mtakumbuka nilizindua barabara ya Mbinga-Mbambay Bay yenye urefu wa kilomita 66 ambayo ni kiunganishi kati ya Bandari ya Mtwara na Mbambay Bay na kwamba jiografia ya Nyasa tuna bandari mbili, pia tulikamilisha ujenzi wa Bandari ya Ndumbi ambayo imekamilika na inafanya kazi.amesema.
Amesema katika ufanyaji kazi wa bandari hiyo, imeweza kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena kutoka tani 40,000 hadi 110,000 kwa mwaka na abiria kutoka 45,000 hadi 100,000. alisistiza kuwa bandari hiyo ni ya kimkakati katika usafiri na kusafirisha mizigo na watu.
Amesema wakati huo, mbali ya bandari, kuna mradi mwingine mkubwa unakwenda Nyasa ambao tayari tafiti za mwanzo zimekamilika
Amesema ahadi nyingine ni Mchuchuma na Liganga maradi ambao watachangia na watu wa upande wa pili.
Pamoja na hayo hatukuzisahau sekta za huduma za kijamii zimekuwa na mafanikio, naomba nigusie kidogo kwenye sekta ya afya hospitali ya wilaya wamo, tumeboresha vituo vitatu vya wilaya na kujenga kipya kimoja na kujenga zahanati 9 mpya, tumeajiri watumishi wa afya 316, ni imani yetu tutaongeza watumishi kadri tutakavyokuwa tunajiri watumishi wa sekta hii,amesema.

Rais Samia alirudia kauli yake kuwa ndani ya siku 100 za utawala kama akipata ridhaa ya kuchaguliwa wataajiri watumisji 5000 ambako Nyasa nako watapata mgawo.
Kwa upande wa elimu amesema wajenga shule mpya 12, sita za msingi na sekondari 6 na chuo cha veta.
Tumejenga veta ili ifundishe vijana wetu waje wafanye kazi kwenye miradi inayoletwa na viwanda vitakavyokuja, kwenye elimu tumefanya hayo na kuendelea na sera bila elimu,amesema.
Kuhusu nishati, Rais samia amesema wamefikisha umeme kwenye vijiji vyote 84, vitongoji 153 vimepta, wakati bado wana kazi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 423 ambapo amewahidi wananchi hao kuwa vyote vitapata umeme.
Pamoja na hayo nafahamu hapa Nyasa kuna changamoto ya umeme kuwa mdogo, tutajenga kituo cha kupooza umeme unaotoka Songea upoozwe kisha usambazwe na hiyo inakwenda kumaliza tatizo la umeme kuwa mdogo, mtavuta wawekezaji wengi,amesema.

Amesema wameendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya barabara ukiwamo ujenzi wa Mto Luhuhu unaounganisha mto Ruvuma, Nyasa na Njombe na kuwa wataendeleza ujenzi wa barabara ya Kidato, Ifakara-Malinzi-Londo hadi Lumecha yenye urefu wa kilomita 512 ambayo inaunganisha mikoa ya Ruvuma na Morogoro.
Tayari tumekamilisha kilomita 61, ni imani yangu kazi iliyobaki itakamilika pale palipobakia. Pamoja na kutekeleza miradi hii na eneo hili natambua mahitaji bado yapo tutahakikisha tunakamilisha miradi inayoendelea inayolenga kufungua wilaya yetu ikiwamo barabara ya Mbamba Bay-Lituhi-Mitomoni, tutajenga daraja la Mitomoni kwenye mto Ruvuma kuunganisha Nyasa na Songea,amesema.
Kuhusu mikopo ya halmashauri amesema kulikuwa na utoaji holela hadi kusimamishwa, lakini baada ya kurudisha wametoka mikopo ya Sh milioni 57 wanatoa mikopo ya Sh milioni 345 kupitia ngazi ya halmashauri.
Kuhusu kilimo awamepongeza wana Nyasa na mkoa mzima kwa kuwa wazalishaji wazuri wa mazao ya biashara na chakula, lakini serikali imejitahidi kutafuta bei nzuri.




