Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia, Nyasa


Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Emmanuel Nchimbi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kwake kuwa mgombea mwenza.


Dk Nchimbi ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Septemba 21,2025 wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho.


Mgombea urais wa chama chetu, nisema mamabo machache kwa kifupi, kwanza nashukuru kwa kunipa heshima ya kuungana nawe katika Mkoa wa Ruvuma na hasa katika eneo la Mbamba Bay. Nitumie nafasi hii kwanza kwa kuwa huu ndiyo mkoa wangu wa nyumbani na mara ya kwanza nazungumza nao wakati huu wa kampeni.


Nitumie nafasi hii kipekee sana kukushukuru mwenyekiti wa CCM kwa heshima na imani kubwa uliyonipa ya kuwa mgombea mwenza wako. Heshima hii si yangu pekee yangu, bali ni heshima kwa mkoa wote wa Ruvuma tunakushuruku sana.


Nitumie nafasi hii kukuhakikishia kwa mila zetu watu wa mkoa wa Ruvuma, imani huzaa imani, nitakusaidia kwa uwezo wangu wote na kwa uaminifu wangu wote kuhakikisha wanatekeleza Ilani ya CCM kama ulivyokusudia, lakini pia unafikia maono yako ya kulikomboa taifa letu kutoka kwenye hali duni na kuwa hali bora zaidi, nitakuwa msaidizi wako mwanamifu na kwa nguvu zangu zote,amesema.


Amesema suala la pili katika kuzungumza kuomba kura aligawiwa maeneo ya kupita kama msaidizi wake, amefanikiwa kupita mikoa 11.


Nimepita mikoa 11, naomba nikupe salamu za mikoa hii, mikoa yote imenituma nikwambie kwamba utashida wewe na CCM kwa kishindo, mikoa yote imenituma nikwambia wabunge wote wa CCM watashinda kwa kishindo, madiwani watashinda kwa kishindo na Rais wao kipenzi atashinda kwa kishindo.


Kwa niaba ya ndugu zetu wa Ruvuma, tunakushukuru sana kwa maendeleo makubwa uliyofanya si kwa Ruvuma tu, bali kwa Tanzania nzima, uwezo wako wa kutafuta rasimali, kusimamia mgawanyo wake na uwezo wako wa kusimamia kila pembe ya nchi yetu inapata maendeleo bila ubaguzi ndiyo inafanya wana CCM tusimame kifua mbele kukinadi chama chetu.

“Nawaomba wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wote tunapiga kura Oktoba 29 na kura za heshima kwa rais wetu, kura ambazo zitampa nguvu ya kuendelea kututumikia, kura ambazo zitaonyesha dunia nzima kwamba tunaimani na mapenzi ya dhati na Rais wetu na tuko tayari kuendelea kufanya naye kazi” amesema.