Kiongozi wa upinzani aliyewahi uwa makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar amefikishwa mahakamani Jumatatu 22.09.2025. Machar anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhaini.

Makamu huyo wa zamani wa Rais Anatuhumiwa pia kwa kuamuru mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo dhidi ya kambi ya jeshi ambapo kulingana na Serikali wanajeshi 250 waliuawa.

Chama cha Riek Machar hivyo kimekanusha tuhuma hizo kikisema ni sehemu ya mpango wa Rais Salva Kiir wa kuutenga upinzani. Wafuasi wa Machar wanasema tuhuma dhidi yake zinaonesha makubaliano ya kugawana madaraka yamekufa na wameitisha mabadiliko ya utawala.