Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, MJaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ameendelea na ziara ya kutembelea mikoa ya Mbeya, Iringa na Dodoma kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa za majimbo hayo kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hizo.
Akizungumza na vyombo vya habari akiwa Mkoani Iringa leo, Jaji Mwambegele amesema maandalizi yanakwenda vizuri na mikoa yote nchini ikiwemo ya Tanzania Zanzibar wameshaanza kupokea vifaa mbalimbali vya uchaguzi.Mroki Mroki – INEC

Kwa upande wake Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa wa Iringa, Ndugu Nuru Sovella amesema mapokezi ya vifaa kwaajili ya mafunzo na vile vitakavyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu yanakwenda vizuri.
Jaji Mwambegele katika ziara yake hiyo katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Dodoma anapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi kwa wagombea mbalimbali wa Kiti cha Rais, Ubunge na Udiwani katika maeneo anayo pita.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu huku kaulimbiu ikiwa ni “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”

