Na Kulwa Karedia-Jamhuri Media-Mwanza
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amesema Mkoa wa Mwanza umepata Sh trilioni 5.6 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ametoa kauli hiyo wakati akihutubia maelfu ya wananchi kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani leo Oktoba 8, 2025.
Amesema fedha hizo ni nyingi mno kwenda mkoa mmoja, jambo ambalo linamefanya kuonekana kwa maendeleo makubwa ambayo sasa yanaonekana kila kona ya mji huo.

Fedha hizi zimesaidia kuwekeza kwenye sekta za mbalimbali, naomba nianze na sekta ya afya ambayo tumefanya vizuri na tunaendelea kuiboresha kila wakati.
Kwa upande huu hiki ndiyo kipaumbele chetu ndani ya serikali ya CCM, sasa ndani ya mkoa huu pamoja na kuboresha hospitali za halmashauri, zanahati tumefanya maboresho makubwa sana, sasa hivi hospitali mbiili za rufaa pale Seko Toure tumejenga jengo na mama na mtoto lenye ghorafa tano kwa gharama ya shilingi milioni bilioni moja na zaidi likiwa na uwezo wa kubeba vitanda 261 kwa wakati mmoja.
Ndiyo maana kwa kiasi kikubwa tumeweza kupunguza vifo vya kina mama na watoto wachanga, pia tumeweka vifaa vya kisasa vikiwamo mashine ya CT SCAN ziko mbili na mtambo wa uzalishaji gesi ya oksejeni.
Zamani tulikuwa tuna safirisha mitungi huko inakozaliwa na kupeleka kwenye hospitali zetu, sasa hivi hospitali zaote za rufaa na mikoa zinazalisha oksijeni,amesema.
Amesema hivi sasa wagonjwa wote wanaozidiwa hospitalini hapatiki taabu ya kupata huduma kutokana na mashine hizo kuwa hospitalini hapo hapo.

Amesema katika hospitali ya Bugando, wamepeleka zaidi ya sh bilioni 9 kwa ajili ya kuboresha huduma, kupeleka vifaa tiba na kufanya ujenzi wa wodi ya wagonjwa mahututi au mahitaji maalumu.
Pia tumejenga jengo la matibahu ya ugonjwa wa kansa au saratani na kununua mashine za uchunguzi wa saratani za matatiti ambazo zitawasaidia watu mbalimbali, tena kina mama wanaweza kwenda kuchunguza saratani ya matiti kuona kama kuna shida unawahi kupata tiba. Tumenunua mashinde za mionzi ya saratani, sasa wagonjwa wa saratani kutoka kanda ya ziwa hawalazimiki kwenda hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam kupata matibabu,amesema.
Amesema kutokana na hospitali hizo, serikali imefanikiwa kuongeza idadi kuhudumia wagonjwa kutoka 1,200 mpaka 1500.
Kwa ujumla tunataka huduma zote za kibingwa zote zipatikane Mwanza, tupunguze rufaa kwenda Dar es Salaam na kwingineko, mkitupa ridhaa yenu tufanya makubwa zaidi.

Katika kisiwa cha Ukerewe tutaboresha hospitali ya Nansio na kuboresha majengo ya wagonjwa wa dharura na kujenga hospitali ya rufaa wilayani humo. Yale mambo sasa mgonjwa kazidiwa kivuko kimeondoka, mgonjwa hana huduma hapana tena, lazima apate huduma hapo hapo,amesema.
Kuhusu elimu, Rais Samia anasema serikali imefanya kazi kubwa ya kujenga shule za msingi na sekondari na kutekeleza sera ya elimu bila ada wamejenga vyuo vitatu vya VETA katika wilaya za Magu, Misungwi na Buchosa.
Hii ni hatua ya kuhakikisha kila wilaya inapata chuo kinachowezesha vijana kupata ujuzi wao kwa kujiajili au kuajiliwa,amesema.
Kuhusu elimu ya juu katika mkoa huo, serikali imejenga Kampasi ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) katika wilaya ya Ilemela na Kampasi ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania iko wilayani Misungwi.
Mballi na hilo, tumeboresha Chuo cha Maendeleo ya Michezo-Malya kilichopo Kwimba, kwani sekta ya michezo ni chanzo muhimu cha ajira kwa vijana wetu, tumekweza zaidi ya shilingi bilioni 34 ili tuzidi kukuza vipaji na kuandaa walimu wengi zaidi katika shule zetu,amesema.
Kwa upande wa nishati, Rais Samia amesema kila sehemu mbalimbali alizopita watu wanasema nishati si tatiz tena kutokana na kumaliza vijiji vyote Tanzania na kugeukia vitongoji.
Anasema jambo kubwa sasa ni nishati ya safi ya kupikia ambayo kila Mtanzania anapaswa kuitumia.

Ndugu zangu kina mama wa Mwanza tuliotoa mitungi ya ruzuku inaonekana wamenogewa, hatuwezi kwenda tena yote kwa ruzuku kama awali, tulitoa kwa ajili ya kuhamasisha kuonyesha nishati safi ya kupikia ndiyo ukombozi wetu kina mama. Kwa yale maeneo ambayo yako nyuma sana, tutakwenda tena kwa ruzuku, kwa maeneo ambayo wameishaelewa nishati hii ndiyo ukombozi tuendelea nayo.
Lakini kwenye umeme kuna ujenzi wa vituo si Mwanza tu bali kanda ya ziwa, tunataka umeme upatikane saa zote na uwe wa kutosha,amesema.
Kuhusu miundombinu, Rais Samia amesema serikali imekamilisha ujenzi wa barabara ya Buhongwa-Igoma yenye urefu wa kilomita 14, lakini bado kuna kazi kubwa mbele kwa sababu miradi mingine inaendelea.
Tumetangaza tenda ya barabara ya Buhongwa-Usagara ambayo itakwenda kwa njia na barabara ya mwendokasi katikati, najua bado kuna barabara za mitaani zinazohitaji fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo.
Katika wilaya mbalimbali kuna babaraba ambazo tumeziweka kwenye Ilani ya uchaguzi tunakwenda kuzijenga kwa kiwango cha lami, lengo letu ni kuunganisha wilaya zote na makao makuu ya mkoa, kata na maeneo mengine.
Miradi ya baraabara ni ya ghali mno maana kilomita moja ya barabara iatoa vituo viwili vya afya na watumishi kwa hiyo mtaona ni gharama kweliweli. Ndiyo maana kwenye eneo hili hamna kazi kubwa kama ile watu wanavyoitarajia, lakini kwa sababu tumemaliza kazi za maji, umeme hili linawezekana,amesema.
Amesema mwelekeo mkubwa wa serikali ni kwenye baraabara mbalimbali nchini zilizomo kwenye ilani zitajengwa na zile zilizoombwa zitaangaliwa uwezekano wa kujengwa.
Kuhsu mradi wa Daraja la JPM, Rais Samia amesema limerahisisha usafiri wakazi wa mji huo na maeneo mengine tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Katika hatua hii nizungumzie maeneo mengine matatu makubwa, mosi ni ujenzi wa reli ya SGR tunaendelea na ujenzi wa kipande cha Mwanza-Isaka cha kilomita 314 kinagharimu shilingi trilioni tatu kimefikia asilimia 63.
Mkoa huu utakuwa na vituo vitano vya abiria ambavyo ni Mwanza mjini, Fela, Bukimbwa na Malya, hivi ni vituo vya kushusha na kupakia abiria, ni maeneo ambayo yatakuwa na shughuli za kiuchumi, hoteli kwa sababu kuna watu wataka waondoke asubuhi watahitaji kulala ni kazi yenu kuchangamkia fursa hizi, wekeni maduka na mambo mengine.
Sisi serikali tutajenga maghala ya kuhifadhia bidhaa ambazo zitasafirishwa kwenda maeneo mbalimbali ndani au nje ya nchi. Hii ni fursa kubwa kaeni mkao wa kula. Pale Fela pana bandari kavu ni jambo jingine ambalo litaleta fursa za ajira kwa vijana wetu,amesema.
Amesema mpaka sasa serikali imekamilisha ujenzi wa vipande viwili vya kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Kule mambo ni safi san asana, kuna watu wanakwenda kazini Dodoma asubuhi na jioni wanarudi Dar es Salaam, reli hii ina manufaa makubwa sana. Tutakapokamiliza au kuunganisha Dar es Salaam mpaka Mwanza unaweza kwenda Dar es Salaam kwa saa 8 mpaka 9, hii itarahisisha biashara pia mzigo ambao mfanyabiashara angeusubiri kwa siku mbili aupokee Mwanza anapokea siku hiyo hiyo, tuoombeane na tuichague CCM ije imalizie kazi hii ambayo tumeianza,amesema.
KWA TAARIFA ZAIDI SOMA GAZETI LA JAMHURI TOLEO LIJALO