Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Mwanza, Boniphace Mkoaba ameamua kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mkoba amepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha Rose Migiro mbele ya mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo Oktoba 8, 2025.


Amesema amefikia uamuzi huo, baada ya kuridhishwa na utendaji kazi mzuri wa chama katika masuala ya maendeleo yanayoonekana machoni kwa Watanzania.
Amesema ametimiza ndoto yake na kuachama na chama ambacho kila kukicha kinahimiza vuruguru zisizokuwa na tija, hivyo ameona ni wakati sahihi wa kujiunga na CCM kutokana na kubeba matarajio makubwa ya Watanzania.