Mgombe wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amesema CCM imeendelea kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika misingi ya utawala bora.

Dkt. Samia amesema katika kumuenzi Hayati Mwl. Nyerere hatuwezi kumtenganisha na misingi ya kiitikadi na kifalsafa aliyoijengea nchi yetu ambayo ilibebwa na dhana kama vile uhuru na umoja, kujitegemea, kazi pamoja na wajibu na dhana zingine muhimu za kiitikadi ambazo alikuwa akizitoa kila baada ya muda katika kuijenga nchi yetu ya Tanzania.

Aidha, Mgombea Urais Dkt. Samia amesema hayo yote yalilenga kujenga Taifa imara linalojitegemea na kujenga maendeleo ya watu ambapo amesema Mwl. Nyerere alisisitiza kuwa maendeleo yote yenye maana hayana budi kuwalenga watu na ndicho ambacho katika dira na mipango yote ya maendeleo na hata kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndani yake zimejielekeza kujenga Taifa linalojitegemea lenye uchumi jumuishi na ustawi wa watu.

Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 10 Oktoba 2025 mbele ya maelfu ya Wananchi wa Butiama mkoani Mara waliojitokeza katika viwanja vya Mwenge ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Urais kupitia CCM.

𝙈𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙚 𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝙖𝙢𝙞𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙤 𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙫𝙪 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙖 𝙠𝙪𝙞𝙣𝙪𝙖 𝙐𝙩𝙪 𝙬𝙖 𝙠𝙞𝙡𝙖 𝙈𝙩𝙖𝙣𝙯𝙖𝙣𝙞𝙖