Na Ruja Masewa, JamhuriMedia, Mbeya

‎Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amezitaka taasisi za fedha kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana ili wawe na Uwezo wa Kuirejesha.

Majaliwa amesema hayo leo tarehe 10/10/2025 mkoani hapa wakati akizindua maadhimisho ya wiki la vijana la kitaifa yanayofanyika viwanja vya uhindini mkoani hapa yakiwahusisha Viongozi wa Chama na Serikali na Wadau mbalimbali.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Majaliwa amezitaka taasisi za fedha za binafsi, umma na mashirika ya fedha, kutoa mikopo ya riba nafuu kwa Vijana, ili wawe na uwezo wa kurejesha bila kukwama.

Hata hivyo amezitaka Halmashauri zote nchini kuendeleza kutoa mikopo nafuu ikiwemo ile ya asilimia 10 ya Mapato kwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

Aidha amewataka Wadau mbalimbali kuhakikisha wanaongoza jitihada za kutoa ushauri wa kibiashara kwa vijana ili waweze kunufaika na mikopo hiyo wanayoweza kumudu kuirejesha kwa wakati.

Maadhimisho hayo ambayo hufanyika kwa siku saba (7) kuanzia Agosti na kumalizika Oktoba kila mwaka huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kilele cha kuzima Mwenge wa Uhuru na kumbukizi la Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mambo mengine yaliyoanikizwa na maadhimisho hayo ni pamoja na utoaji wa zawadi kwa washindi watano (5) wa shindano la Insha lililoandaliwa na shirika la utangazaji la Tanzania (TBC), ambapo washindi walipata Komputa mpakato na fedha TASLIMU Sh. 1,000,000 na zawadi.

Maadhimisho hayo yanataraji kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba ambapo Mgombea Urais Dk. Samia Samia Suĺuhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mbio za kuuzima Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa sokoine jijini hapa.