Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 26 ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Mwalimu Baba wa Taifa Julius Nyerere, klabu ya madaktari kwa kushirikiana na klabu mbalimbali za michezo, wasanii wa ngoma za asili na wadau wengine kutoka katika maeneo mbalimbali hapa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kufanya usafi.

Wadau hao wameshiriki sehemu ya kwanza ya maadhimisho hayo kwa kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Songea (Homso) pamoja na soko kuu la Songea.

Akizungumza mara baada ya kumaliza shughuli za usafi Kaimu Matibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankoo amewataka wananchi wa manispaa ya Songea kutumia maadhimisho hayo kila moja ajitume kufanya kazi kwa bidii huku akisisitiza kuwa hayati mwalimu Nyerere ambaye ni mwasisi wa demokrasia nchini aliwahimiza Watanzania kuzingatia Demokrasia.

Aidha kaimu Katibu tawala huyo Mwankoo amewasihi wananchi kila mmoja ajitokeze kwenda kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk. Luis Chamboko ameeleza umuhimu wa usafi kuwa ni wananchi wakizingatia usafi watajiepusha na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya ngozi, kuhala na kutapika.