Na Mwandishi Wetu,Jamhuri lMedia,
Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda ameipongeza Serikali kwa Miaka minne ameongeza bajeti ya kilimo kwa viwango kikubwa hadi kufikia Tsh 1.2 Trilion licha ya Kuwepo kwa Changamoto kubwaa ya uzalishaji pamoja na Masoko.

Amesema hayo Leo Oktoba 13,2025 Jijini Dar es salaam katika Ufunguzi wa kongamano la miaka 25 ya Asasi ya kusaidia Sekta binafsi ya kilimo Private Agricultural Sector Support (PassTrust )tangu kuanzishwa kwakwe kwa lengo la kuwania Wananchi kupitia Kilimo pamoja na mnyororo mzima wa thamani kwenye masuala ya kilimo,Uvuvi na ufugaji.

“Tuna Changamoto kubwa ya uzalishaji,lakini pia tuna Changamoto nyingine ya Elimu ya kilimo,Uvuvi na ufugaji,tunatambua kwamba hizi ni sekta rasmi sana ambazo Jamii ya Kitazania inaziona kama sio rasmi sana”Amesema Mapunda

Nakutoa wito kwa kupitia Pass na taasisi zingine kuongeza kutoa elimu kwa Jamii kuona kilimo kama tu kua meneja wa benk,Kilimo ni kikubwa zaidi kwa sababu unapata hapohapo uliopo na jinsi tunapoelekea huko trend ya dunia inatuonesha hitaji la chakula Duniani linaongezeka mara kwa mara.

Aidha amesema kuwa Jamii itakavyojiweka vizuri katika utunzaji wa mazingingira pamoja na kuongeza mazingira wezeshi ya Serikali kwenye kufanya uwekezaji wa bajeti kubwa,miundombinu ya barabara,reli na ufanisi wa bandari kwenye Sekta ya kilimo,Uvuvi na ufugaji ndani ya muda mfupi Tanzania itakuwa mbali kiuchumi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Biashara kutoka Pass Trust Adam Kamanda amesema kwamba kikao cha leo kimehusanisha Wadau wote wanaoshiriki katika dirisha la Kilimo,Uvuvi na ufugaji katika taasisi za kifedha.

Pass Trust imeanzishwa Mwaka 2000 na ubia katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mfuko wa Waziri Mkuu pamoja na Serikali ya Dernmak Ikiwa lengo lake kuu ni kuchochea Kilimo Biashara ili Taasisi za fedha ziweze kuongeza uwekezaji katika Sekta ya kilimo,Uvuvi na Mifugo,pamoja na mazao ya misitu.

“Leo tupo kwenye kongamano hili kubwa ambalo tumelifanya Nchi nzima,na tupo kwenye kilele katika Mkoa wa Dar es salaam ikiunganisha pwani, Morogoro, Dodoma pamoja na Zanzibar,na tumetoka kufanya kikao kama hiki tukiwaunganisha Taasisi zote za fedha ambazo zinakopesha Wakulima Nchi mzima,kwa hiyo wale wafanyakazi wote kwenye madirisha hayo tumewaunganisha pamoja kama Wadau ili kujadili fursa na njia bora ya kukopesha katika Sekta ya Kilimo.

Nakuongeza kuwa”tumemaliza kufanya kongamano kama hili katika Mkoa wa Njombe,Arusha Moshi,Kahama,Bukoba na leo tupo Dar es salaam katika Kanda zetu sita, Pass Trust hadi sasa katika Sekta ya kilimo imeweza kutoa dhamana zenye takribani trioni 2.4 katika kipindi cha miaka 25,tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika miaka ya hivi karibuni tumeona Kilimo katika bajeti ya Sekta kimeongezeka sana kufikia trioni 1.2 bajeti mzima ya Wizara ya kilimo.

Nae Meneja uhusiano Coop Bank Tanzania upande wa vyama vya ushirika pamoja na Kilimo Khadija Seif amesema kuwa kwa mara ya Kwanza benk hiyo Mpya imeingia uhusiano na Pass Trust kwa ajili kutoa mikopo Kwa Wakulima,Wavuvi na Wafugaji.

“Kama mnavyojua Tanzania changamoto kubwa kwenye Kilimo bila kupata backup ya Pass mikopo unakua sio mizuri,hivyo tunafanya kazi na Pass,taasisi hii imekuwa nzuri Sana kwasababu Toka tumeanza mwezi WA nne Mwaka huu tuna portifalia ya shilingi bilioni nane ambayo ipo covered na Pass, tunaishukuru sana uwepo wao unasaidia wakulima wengi kunufaika hapa Tanzania”amesema.