Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Doto Mashaka Biteko amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono na maelekezo yaliyowezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wilayani, mkoani na Taifa kwa ujumla.
Dkt. Doto Biteko amesema hayo mbele ya Mgombea Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika Wilaya ya Bukombe, ikiwa ni sehemu ya Kampeni zake Mkoani Geita Oktoba 12, 2025.

“ Mgombea umetufundisha mengi, kupitia kauli mbiu yako ya kazi na utu tunasonga mbele, unatenda zaidi na kusema kidogo. wewe unazungumza matatizo ya watu na maisha yao wakati wote, Utu kwako ni kipaumbele na Kazi kwako ni msingi wa maendeleo” amesema Dkt. Biteko
Ametaja miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwemo Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, Daraja la JPM, Barabara za lami ndani na nje ya Wilaya ya Bukombe pamoja na taa za barabarani ili kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa Biashara.
Dkt. Biteko pia amemshukuru Dkt. Samia na kuahidi kuendelea kuwa msikivu, mwaminifu mwadilifu ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji katika nafasi yake ya usaidizi.




