Na Stella Aron, JamhuriMedia,Tanga

Tanzania ina zaidi ya kilomita 1,400 za pwani pamoja na eneo la uchumi wa bahari lenyeukubwa wa takriban kilomita zamraba 223,000.

Rasilimali hiikubwa ya bahari ni msingi muhimu wa shughui za kiuchumi kama vile uvuvi endelevu, usafirishaji wa bahari, utalii wa pwani, nishati ya bahari, pamoja na uvunaji wa viumbe wa baharii kwa njia rafiki waazingra.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa sekta ya uvuvi inatoa ajira kwa watu zaidi ya milioni 2.5 nchini na huchangia asilimia 1.5 ya pato la tafa.

Pamoja na fursa hizolukuki bado, matumizi yake hayajafiiakiwango cha kuridhisha, hasa katika maee ya Bara tofauti na Zanzibar ambako zaidi ya asilimia80 ya fursa za uchumi wa buluu inatumika ipasavyo kutokana na sera za wazi na utekelezaji madhubuti unaofanywa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Ili kurejesha uhifadhi na urejeshaji mazingita ya pwai husasusan Baharii ya Hidi, Mradi wa Pwani Yetu umelenga kutoa elimu kwa jamii ili kujua faida mbalimbali zitonakazo na kulinda na kutunza mazingira ya bahari.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limeuona umuhimu huo na kuamua kutekeleza mradi wa Pwani Yetu wenye lengo la kulinda mazingira ya bahari na pwani sanjari na kukuza uchumi kwa wananchi wanaoitumia bahari kujipatia kipato.

Mshauri wa mradi huo kutoka GIZ, Dkt. Robert Katikira anasema mradi huo umekuwa chachu kubwa katika kuchochea ili kuikoa bahari ambayo inakabiliwa na uharibifu unaotokana na shughuli za binadamu.

Katika kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana GIZ kwa kushirkiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), pamoja na Taasisi binafsi ya Nukta Afrika yenye makao makuu yake Dar es Salaam wameungana a kutoa elimu ya waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kuitunza bahari.

Mradi huo unalenga kuhudumia sehemu ya kilomita za mraba 1,424 za Pwani ya Tanzania bara huku mikoa ya Tanga, Lindi na Mtwara ikihusika moja kwa moja.

“Mikoa mitatu ya Tanga, Lindi na Mtwara ndiyo itakayonufaika hivyo waandishi wa Habari ndio sikio na mdomo wa kusikia na kuwaelimisha wananchi kupitia kalamu zenu.

“Tunaamini kuwa kama waandishi wa habari wakielewa zaidi inakuwa rahisi sana kuelimissha jamii kwa mapana zaidi na taarifa hufika haraka na katika maeneo mbalimbali na kufika kwa haraka.

“Mafunzo ya uhifadhi wa bahari na pwani yanapaswa kuwa endelevu, hatua hiyo itasaidia kuiokoa bahari na uharibifu unaofanywa na binadamu,” anasema Katikira.

Anasema kuwa GIZ, Nukta Afrika na JET, kwa pamoja wamewakutanisha waandishi wa Habari za Mazingira zaidi ya 30 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini na wataalamu wa masuala ya uhifadhi wa bahari na kuwapa mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika jijini Tanga.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Jestina Katandukila anasema kuwa mazingira ya baharini na ukanda wa pwani ni rasilimali muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.

Maeneo haya yanajumuisha miamba ya matumbawe, bahari kuu, mikoko, fukwe na maeneo tambarare ya pwani ambayo ni makazi ya viumbe wengi. Mazingira haya hutoa huduma muhimu kama chakula, ajira, burudani, pamoja na kusaidia kudhibiti mabadiliko ya tabianchi ambapo viumbe wa baharini wanaanzia kwa viumbe wadogo kama planktoni hadi samaki, pomboo na nyangumi.

“Mazingira haya ni chanzo kikuu cha samaki na mazao mengine ya baharini yanayochangia usalama wa chakula duniani. Pia hutoa fursa za nishati mbadala kutoka kwenye mawimbi na mikondo ya bahari” anasema Dk Jestina.

Ukanda wa pwani, ikiwa ni kiunganishi kati ya bahari na nchi kavu, una misitu ya mikoko, matumbwiga ya chumvi, na mito inayoelekea baharini. Maeneo haya ni mazalia ya viumbe wengi, hususan samaki na kamba, na ni sehemu muhimu ya utalii wa kiikolojia.

Anasema kuwa zaidi ya chakula, mazingira ya baharini na pwani hutoa huduma za kisayansi. Watafiti wengi wanatumia viumbe wa baharini kugundua dawa mpya na teknolojia ya kisasa. Hii inaongeza umuhimu wa kuhifadhi bayoanuwai kwa ajili ya maendeleo ya baadaye na uwezo wa kupambana na magonjwa na mabadiliko ya mazingira.

Hifadhi ya mazingira haya pia inaleta faida za kiuchumi. Uvuvi endelevu huongeza kipato cha jamii za pwani na kuchangia pato la taifa. Utalii wa baharini, kama vile kupiga mbizi na kutazama matumbawe, ni vyanzo vya ajira na mapato kwa maelfu ya watu.

Hata hivyo, mazingira haya yanakumbwa na changamoto nyingi kama uvuvi haramu na uliozidi kiwango hufifisha idadi ya samaki na kuhatarisha uhai wa viumbe wa baharini. Uharibifu wa makazi, hasa ukataji wa mikoko kwa ajili ya kilimo au ujenzi wa hoteli, husababisha mmomonyoko wa pwani na kupotea kwa makazi ya viumbe.

Uchafuzi wa bahari kutokana na majitaka na taka ngumu, hususan plastiki, huathiri afya ya viumbe na ubora wa maji. Aidha, mabadiliko ya tabianchi yameongeza joto la bahari na kusababisha matukio ya kufa kwa matumbawe (coral bleaching), ambayo ni mazalia muhimu ya samaki.

Anaongeza kuwa Tanzania imechukua hatua madhubuti za kuhifadhi mazingira haya kupitia Hifadhi za Baharini, maeneo kama Mnazi Bay-Ruvuma Estuary Marine Park na Mafia Island Marine Park yamelindwa dhidi ya uharibifu. Pia, kuna maeneo yanayosimamiwa na jamii kama Kigombe na Tanga Marine Reserves.

Lengo la kimataifa la 30×30 linahimiza kulinda asilimia 30 ya maeneo ya bahari ifikapo mwaka 2030.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojitolea kutekeleza lengo hili kupitia mikataba ya kimataifa kama CBD na COP26. Lengo kuu ni kusitisha upotevu wa bayoanuwai na kuimarisha uthabiti wa mifumo ya ikolojia” anasema.

Hata hivyo anasema kuwa ushirikishwaji wa jamii umeonekana kuwa suluhisho muhimu katika maeneo yanayosimamiwa na jamii ambapo wavuvi wanaweka kanuni za uvuvi endelevu, kama kufunga uvuvi wakati wa msimu wa kuzaliana, kutumia nyavu zenye matundu makubwa, na kilimo cha mwani kama mbadala wa kipato.

Aansema kuwa Tanzania pia imewekeza kwenye elimu na utafiti kwa kuhusisha taasisi kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambacho hutoa mafunzo ya ekolojia ya bahari na usimamizi wa rasilimali za pwani. Utafiti huu huchochea uvumbuzi na kusaidia sera bora za uhifadhi.

Katika maeneo kama Rufiji Delta, mikoko inarudishwa kwa upandaji wa miti ili kuimarisha kinga dhidi ya mafuriko na kuendeleza uvuvi wa kamba. Vilevile, utalii wa baharini unaendeshwa kwa njia ya kiikolojia ili kulinda mazingira na kuwapatia wakazi kipato mbadala.

“Mabadiliko ya tabianchi yameleta madhara kama kupungua kwa samaki, mmomonyoko wa pwani, na kupotea kwa makazi ya viumbe. Katika maeneo kama Zanzibar, zaidi ya asilimia 50 ya matumbawe yameathirika kutokana na kuongezeka kwa joto la bahari” anasema.

Kupitia uchumi wa buluu, Tanzania ina fursa ya kutumia bahari kwa ajili ya maendeleo bila kuiharibu. Sekta kama uvuvi, utalii, nishati mbadala na usafiri wa baharini zinaweza kuchangia uchumi ikiwa zitadhibitiwa kwa uendelevu.

Teknolojia pia ina mchango katia vyombo vya kisasa vya kufuatilia uvuvi, matumizi ya data kutoka kwa jamii za wavuvi, na kampeni za elimu zimesaidia kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira ya baharini ambapo kwa Zanzibar, kilimo cha mwani kinachofanywa na wanawake kimeboresha maisha yao na kulinda mazingira.

Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Afrika, Nuzulack Dausen ambaye alitoa elimu ya namna ya uandishi wa habari wenye tija ikiwa ni pamoja na kutokwepa kutmia Tekolojia ya Akili Mnemba.

“Matumizi ya teknolojia ya akili Mnembe hayakwepeki hata hivyo ni vyema kuongeza umakini wa majibu yanayopatikana wakati wa matumizi ya AI’ anasema Nuzulack.

Anasema kuwa waandishi wa habari wa mazingira wana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mazingira ya bahari yanalindwa hivyo ni vyema kuandika habari zenye kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa kulinda mazingira kwa ajili ya faida ya kizazi kijacho na maendeleo ya nchi.

Naye Mkurugenzi JET, Chikomo anasema kuwa mazingira ya baharini na pwani si tu rasilimali, bali pia ni msingi wa maisha na ustawi wa jamii ambapo uendelevu wa rasilimali hizi utategemea kiwango cha juhudi tunazoweka sasa katika kuyalinda dhidi ya uharibifu.

Kwa msingi huo, kila mdau kutoka kwa wavuvi hadi kwa watunga sera anapaswa kushiriki kikamilifu katika juhudi hizi ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na bahari na ukanda wa pwani kwa vizazi vijavyo.

“Mazingira ya Bahari nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu hivyo katika juhudi za kuleta mabadiliko dhidi ya uharibifu wa mazingira ya bahari kila mmoja anapaswa kusimamia suala hili kwa ajili ya faida ya nchi lakini pia kwa kizazi na kizazi na kwa maendeleo ya uchumi wa buluu” anasema.

Mradi wa Pwani Yetu ni mpango wa kijamii unaolenga kuboresha ustawi wa jamii za pwani nchini Tanzania, hasa katika mikoa kama Tanga, Lindi na Mtwara.