Na Mwandishi wlWetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kwa kushirikiana na Mamlaka
zingine za kisheria 3 ,Oktoba hadi 10 , 2025 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha “Televisheni mtandao” bila kuwa na leseni.
Waliokamatwa ni 1. Japhet Alex Thobias Mkazi wa Sabasaba Ukonga 2. Joseph Augustino Mabwe Mkazi wa Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV, 3. Tegemeo Zacharia Mwenegoha Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na 4. Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA TV.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 15,2025 Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema kuwa upelelezi umekamilika na mifumo mingine ya kisheria itatumika ili
watuhumiwa wote wafikishwe mahakamani haraka kadri itakavyowezekana kujibu tuhuma zinazowakabili.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi zao kwa
kuzingatia mifumo ya kisheria na halitasita kuwatia mbaroni wanaotuhumiwa kutenda makosa.
Aidha Jeshi la Polisi limesema linajidhatiti kuimarisha hali ya usalama Oktoba 29, mwaka huu siku ya Uchaguzi Mkuu hivyo wananchi wakatize haki yao kikatiba waende wakapige kura.
