Mpango azima Mwenge na Kuzindua Kitabu chake

Na Ruja Masewa, JamhuriMedia, Mbeya

Makamu wa Rais Dk. Philipo Mpango amezima rasmi Mwenge wa Uhuru na Kuzindua Kitabu chake cha Historia ya Miaka 61 ya Mbio hizo yaliyofanyika mkoani hapa jana Oktoba 14, 2025.

Sherehe hizo zilihusisha Maadhimisho ya Kumbukizi la kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Miaka 61 ya Mbio hizo.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Dk. Mpango amesema, Mwalimu Nyerere ni Kielelezo na Alama isiyofutika ya Utawala Bora, ambaye alihimiza mambo mengi muhimu katika falsafa yake.

Alitaja Mambo hayo kuwa ni, Elimu bure kwa wote, Kujenga Nchi ya Tanzani) yenye Haki, Ujamaa na Kujitegemea na Harakati za Ukombozi wa Kusini mwa mwa bara la Afrika na Afrika yote.

Kuhusu Mwenge alisema, umekuwa chombo muhimu kilichotumika kuwaunganisha watu wa makabila yote nchini, Kuendeleza Lugha ya Kiswahili na Alama ya Uzalendo, Amani, Umoja na Maendeleo.

Aidha aliwataka Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Kauli, Mwenendo, Matendo na Ushauri wake ambapo alirejea na kutaja Fikra zake,

“Sisi tumekwisha kuwasha mwenge,
na kuuweka juu ya mlima, mlima Kilimanjaro.
Umulike hata nje ya mipaka yetu ulete tumaini
Pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali ambapo pana chuki, na heshima ambapo pamejaa dharau.”.alisema Hayati Nyerere.

Juu ya Uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Mbio za Mwenge Mpango amesema, Kitaelezea Safari na Mafanikio ya Mbio hizo katika kuhamasisha maendeleo, kupinga madawa ya kulevya, Malaria, Ukimwi, Lishe Bora na kuimalisha Uzalendo.

Aidha amewataka Wananchi na Vijana, Kujitokeza kupiga Kura Jumatano Oktoba 29, 2025 akiwaomba kukipigia Kura Chama cha Mapinduzi (CCM) na kumchagua Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Mgombea Mwenza Balozi Dk. John Nchimbi, Wabunge na Madiwani wake.

Kwa Upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbali ya Kuwapongeza Wakimbiza Mwenge wakiongozwa na Ally Ussi, amewaasa Wananchi kujitokeza kupira Kura kuwachagua Viongozi Bora na sio Bora Viongizi.

Amewashukuru Viongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa Maandalizi bora ya Maadhimisho hayo na Kumshukuru Mgombea Ubunge Jimbo la Uyole Dk. Tulia Ackson akawaombea Kura za Ubunge yeye na wenzake wakiwemo Madiwani wa CCM wa nchi nzima.

Mbio za Mwenge zilianza Aprili 2, 2025 Kibaha Pwani na kukimbizwa mikoa 31 ya Tanzania, na Halmashauri 155 ukiongozwa na Ussi na Viongozi wenzake Sita (6).