Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
Serikali imetangaza kuanzia Januari 2026 Kima cha Chini cha Mshahara kitaanzia niTsh 358,322 kutoka Tsh 275,060 Ikiwa ni Ongezeko la asilimia 33.4 kwa Watumishi Sekta binafsi
Agizo hilo limetolewa leo Oktoba 17,2025 Jijini Dar es salaam na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira,na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete ambapo Amesema kwa mujibu wa Sheria Kima cha Chini cha Mshahara kimeongezeka hivyo Waajiri wote wazingatie kulipa Watumishi hao.

” Ikumbukwe Serikali ilipandisha Kima cha Chini cha Mshahara kwa Watumishi wa Umma asilimia 35.1 kutoka Tsh 370,000 hadi TSH 500,000 kwa lengo la kuimarisha ustawi wa wafanyakazi hili lilitaƱgazwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Wakati wa MaĆ dhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Meinmosi Mkoani Singida Mwaka huu” Amesema Waziri
Sambamba na hayo amebainisha kuwa tangazo la kupanda kwa Mshahara Kwa mara ya mwisho kwa Sekta binafsi ilikuwa 2022 hivyo tangazo la Leo Mwaka 2025 imefikia Miaka mitatu kwani Sheria unataka kila.baada ya Miaka mitatu ifanyike mapitio na mchakato wa Mshahara wa Kima cha Chini
” Waajiri wote wa Sekta binafsi kuzingatia kutekeleza kima hiki kipya cha Mshahara kwa kuwa ni takwa la kisheria Ofisi yangu haitasita kuchukua hatua kwa Waajiri watakaokaidi au kashindwa kuitekeleza amri hii kwa makusudi” amesisitiza Waziri
Aidha Wizara yenye Dhamana itaendelea kufuatilia kwa karibu Utekelezaji wa amri hii kutoa elimu kwa Waajiri na wafanyakazi pamoja na kufanya tathimini ya mara kwa mara ili kuhakikisha Utekelezaji wake unafanyika kikamilifu.

Naye Rehema Ludanga Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi TUCTA Waajiri wote walio katika Sekta binafsi waangalie ulipaji wao akaendane na jinsi walivyotangaziwa hivyo hivyo na wafanyakazi nao wakawajibike ipasavyo kazini wazalishe
Naye Mwakilishi wa CHama cha Waajiri Tanzania ATE Suzani Ndomba Amesisitiza Mchakato huo walienda kukusanya maoni kutoka kwa Waajiri na wakakubali ulipaji wa Mshahara Kwa Waajiri hivyo watakwenda kutekeleza.
