Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wa Mpanda mkoani Katavi wakati alipowasili katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda ili kuwahutubia wananchi hao na kuwaomba kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wanunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote.