Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Morogoro leo Oktoba 18,2025 kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni ya kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani

Kwa mujibu wa ratiba ya leo,Dkt.Nchimbi atafanya mikutano mitatu. Mkutano wa kwanza utakuwa ni wa kuwasalimia Wananchi katika kata ya Kidoma,Mikumi na mkutano mwingine utafanyika kata ya Mwaya,Kilombero na wa tatu utakuwa Mtimbira,Malinyi.