Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia, Sumbawanga
Mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amefuta tozo na kodi zaidi ya 200.
Mwigulu ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM kwenye uwanja wa Kwiza mjini Sumbawanga leo Oktoba 19,2020.
Amesema Rais Samia amechukua hatua hizo baada ya kuingia madarakani mwaka 2021.
“Ulipoingia madarakani mwaka 2021 ulikuta kuna malalamiko mengi ya tozo na kodi, ukafuta kodi na tozo zaidi ya 200 ambazo zilikuwa zinalalamikiwa na wananchi,”amesema.

Amesema tozo hizo zimefutwa katika taasisi mbalimbali zikiwamo za kidini, kwa wafugaji, wakulima mpaka kwa madereva wa pikipiki (Bodaboda) ambao wameshushiwa faini kutoka Sh 30,000 hadi Sh 10,000,”amesema.
“Ulifuta kodi nyingi, viongozi wa dini wako hapa no mashahidi wanalijua hili, ukaelekeza taasisi zisizofanya biashara ziondolewe hali hii ndiyo maana hivi sasa hakuna tena malalamiko.
“Mhesy Rais ulitoa kibali cha kuwalipa watoa huduma ambao walikuwa wanadai fedha nyingi, ulitoa shilingu trilioni 8 kwa watoa huduma, wakandarasi na watumishi wastaafu wetu ambao ulielekeza sh trilioni 2.Leo hii wazee wetu maisha ya nakwenda vizuri,”amesema.

Amesema Rais Samia amechukua hatua mbalimbali zikiwamo za kukomesha makadirio ya kodi yasiyostahiki ambayo yalikuwa yanafanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Tumekuwa na uhusiano mzuri wa kukufanya mapato kati ya wafanyabiashara na serikali, ndiyo maana mpaka sasa makusnayo yameongezeka kutoka Sh trilioni 1.3 hadi 8 kwa mwezi.
Amesema mapato hayo yamekuwa msaada mkubwa ndiyo maana Serikali imekuwa na uwezo wa kutoa elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita, huku akiongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
“Pamoja na mafanikio haya makubwa ambayo yanaonekana sasa, unakumbuka ulipoingia madaraka ulichukua hatua za kushusha gharama za maisha ya Watanzania ulipoamua kutoa shilingu bilioni 100 kwenye sekta ya mafuta ili kuwapunguzia mzigo wananchi,”amesema.

Amesema katika miaka minne iliyopita, Rais Samia amesaidia kutoa nyingi kwa vijana wengi nchini.
Kuhusu amani, amewasihi Watanzania kulinda amani, mshikamano na umoja ulipo.
“‘Ukiona mtu anakushauri ufanye ubaya, huyo hakutakii mema na haitakii meme nchi yetu, mkatae kabisa, tunataka kuona mambo mazuri yaliyofanywa na wewe yanaendelea kuwasaidia Watanzania ambao wanataka kuondokana na umasikini,”amesema.
Kwa upande wa sekta ya afya, amesema Rais ameweza kujenga zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na rufaa nchi nzima.
Amesema ameweza kusambaza vifaa tiba vikiwamo mashine za CT scan, RMI na nyingine nyingi.
Amesema taasisi za kimataifa zinazopima maendeleo zimeitangaza Tanzania kuwa kinara katika sekta za elimu, afya na barabara.
Amesema mafanikio hayo yamesababisha Benki ya Dunia (WB) kuitangaza kuwa kinara na nchi yenye uchumi imara kwa nchi za Afrika Mashariki.





