Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia
Dar es Salaam

Jumla ya shule 20,517 Wanafunzi wa Darasa la nne Waliosajiliwa Mwaka huu 1,582,140 wanatarajia kufanya Mtihani wa Upimaji wa kitaifa Oktoba 22 hadi 23,2025 ambapo kati ya hao wavulana 764,290 Sawa na asilimia 48.31 huku wasichana wakiwa 817,850 Sawa na asilimia 51.69

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 21,2025 Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Prof Said Ally Mohamed amesema wanafunzi wapato 1,475,637 Sawa na asilimia 93.27 watafanya Upimaji Kwa lugha ya Kiswahili huku Wanafunzi 106,503 sawa na asilimia 6.73 watafanya kwa lugha Kingereza

Hata hivyo amebainisha kuwa Wanafunzi 5,750 wenye mahitaji maalumu kati yao wenye uoni hafifu ni 1,164, na wasioona 111 wenye uziwi 1,161 wenye Ulemavu wa akili 1,641 na wenye ulemavu wa viungo 1,673

“Wanafanyia wa Darasa la nne watafanya masomo 6 ambayo ni Sayansi, Hisabati, Joografia, Mazingira, Sanaa,Michezo, Kiswahili,English Language, Historia ya Tanzania na Maadili pia kutakua Lugha ya Kifaransa,Kiarabu na Kichina na Mwanafunzi atatakiwa kufanya somo Tu kutoka ” amesema Katibu Mtendaji

Katibu Mtendaji amesisitiza kuwa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la nne ni muhimu kwa kuwa huwezesha kufahamu viwango cha Wanafunzi katika kumudu stadi za juu za kusoma ,kuandika na kuhesabu

Hata hivyo maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na kisambaza kwa karatasi za Upimaji pamoja nyaraka zote muhimu zinazohisu Upimaji huo katika Halmashauri /Manispaa zote nchi nzima wasimamizi wote wameshapewa Semina na vituo vimekamilika vyote

Aidha Kamati zote za Mitihani ziweke Mikakati ya kuzuia mianya yote inayoanza kusababisha kutokea kwa udanganyifu na Wasimamizi wote walioteuliwa kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia uadilifu wa hali ya juu.