Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amesema vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa majimbo Kivule, Segerea, Ukonga na Ilala wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu zilizofanyika kwenye uwanja wa Cheka-Kinyereze jijini Dar es Salaam leo Oktoba 22,2025.
“Jambo la mwisho nalotaka kuongea nanyi ni usalama wa raia wetu, niliongea jana, nataka niongee tena leo kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndani ya taifa hili vimejipanga vema, tumevijengea uwezo wa kutosha, tuko salama wakati wowote iwe wakati wa uchaguzi iwe hakuna hakuna uchaguzi tuko salama wakati wote.
Hivi vitisho vidogo vidogo wanavyovifanya kama mnawalewa waulizeni tuko salama wakati, nawatoa hofu wananchi tokeni kapigeni kura tuko salama,amesema.
