Na Kulwa Karedia, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amesema imejipanga vizuri kuboresha makazi ya wananchi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa majimbo ya Kivule, Segerea, Ukonga na Ilala wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu zilizofanyika uwanja wa Cheka-Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 22,2025.

Amesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limekuwa na kazi kubwa ya kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema Tanzania ina uhitaji wa nyumba milioni 3 kwa mwaka mzima na kwa sababu serikali ilikuwa haipunguzi idadi hiyo sasa wanajielekeza kwa nguvu zote.

“Kitaifa Shirika la Nyumba (NHC),limejipanga kutekeleza mipango kadhaa ya makazi, ukiwamo mpango kabambe wa Samia Housing Scheme au Mpango wa kujenga nyumba wameupa jina langu wamejipanga kujenga nyumba 5,000 katika hizo 560 zimekamilika eneo la Kawe.


Pia nyumba 400 zinaendelea kujengwa eneo la Mtoni-Dar es Salaam, nyumba 1,000 ujenzi wake utaanza hivi karibuni katika maeneo mengine nchini ikiwamo eneo la Urafiki-Dar es Salaam nyumba 200 na Dodoma nyumba 800 zitajengwa,tunakwenda vizuri,amesema.

Ndani ya Wilaya ya Ilala, Rais Samia amesema miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara eneo la Kariakoo linaendelea vizuri.

Kama mnavyojua Kariakoo kutokea shida nikaunda kamati ikaenda kuangalia tatizo, matatizo ni makubwa shirika letu linajielekeza pale tuna miradi 16 ya ubia baina ya wafanyabishara na serikali kazi ya kujenga inaendelea,amesema.

Amesema shirika hilo limefanya maboresho makubwa ya nyumba zake nyingi ndani ya wilaya hiyo.

Kuhusu bandari amesema wamefanya maboresho makubwa ikiwamo Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na zingine kwa ajili ya kufanya kazi na nchi za Msumbiji na Malawi.

Kwa upande wa viwanja vya ndege, Rais Samia amesema tofauti na Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, serikali imefanya kazi kubwa kwenye maboresho ya viwanja mbalimbali na kuwa Ilani ya CCM imeelekeza ununuzi wa ndege nane kwa ajili ya kuendelea kulipa uhai Shirika la Ndege Tanzania (ATC).

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameahidi kujenga daraja la kisasa katika eneo la Jangwani na soko la kimataifa katika eneo hilo ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara wengine.


Ndugu zangu tukisema kazi na utu tunasonga mbele, tunatizama utu wa mtu kwenye sekta pamoja na zile za vichocheo vya kujenga utu wake.sekta za vichocheo ni zile zinazokuza uchumi kama miundombinu ya usafiri na usafirishaji, hapa tunazungumzia ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege na uboreshaji wa bandari zetu, vivuko, meli na reli zetu,amesema.

Kwa sisi tuliosoma uchumi, tunaambniwa ,mtu ana mahitaji makuu manne, chakula,maji,nyumba na nguo. Huu ndiyo utuukija kwenye Tanzania kuna mambo tumeyaongeza, sisi kwetu tunasema la kwanza chakula,maji (maji ni uhai), afya ni takwa la msingi la mwanadamu na la nne ni chakula.

“Kwenye chakula lazima kiwe kile kinachopendeza mwananchi, ukienda pale Kisutu utakupata makapu yamejaa mchele kila aina, maharahge, sembe, samaki, nyama wana sehemu yao.

Cha muhimu kwenye serikali ni kuzia mfumko wa bei ili kila Mtanzania ambaye halimi kwa sababu anayelima anacho ndani asiyelima lazima akanunue, lazima tuzuie mfuko wa bei kila Mtanzania aweze kukifikia chakula kwa miaka minne mfululizo toka tulivyotoka kwenye janga la covid mfuko wetu ulipanda mpaka asilimia 6, tumewezesha kuusha mpaka asilimia 3 na huu ndiyo kwenye Ilani yetu,amesema.


Kuhusu sekta ya maji amesema wamefanya vizuri japo hajatosha na lengo ka serikali ni kuhakikisha miaka mitano ijayo kila Mtanzania anapata maji safi na salama.

Kuhusu suala la afya, Rais Samia amesema kazi bado inaendelea hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sababu ni kitovu kikubwa cha hospitali kama Muhimbi, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Ocean Road.

Kwa msingi huo tumejipanga kufanya makubwa, kipindi hiki tumeweza kujenga na kuboresha hospitali za rufaa za kanda na hospitali za rufaa za mikoa ili kuhakikisha watu watakapopata changamoto za kiafya wanashughulikiwa mara moja ili kuondoa msongamano katika hospitali zetu kubwa.

Tumejitahidi sana, hatujamaliza Tanzania watu tunazaliana, tunakuwa mahitaji ya afya yanaendelea , tutaendelea kufanya kazi mpaka tuhakikishe alivyosema ndugu yangu Wenje (Ezekiah) kuwa hapa kikomo, tumepiga hatua tunafanya mambo makubwa sana,
Miaka mitano au sita iliyopita, Tanzania tulikuwa hatufanya upasuaji wa matundu ya mioyo leo tunafanya, hatukuwa tunapandika uroto kwenye mgongo leo tunfanya hivyo, Tanzania tunapandikiza figo, tunafanya upasuaji mkubwa ambao tulikuwa tunapeleka wagonjwa nje sasa tunaweza kuokoa fedha zetu za kigeni na kuzihifadhi zifanye mambo mengine, hatujamaliza tutaendelea makubwa yamefanyika,amesema.