Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,
Dar es Salaam
Chama cha NCCR Mageuzi Kimesema amani na mshikamano ni utajiri Mlmkubwa kuliko dhahabu almasi, vito vya thamani hivyo kila Mtanzania ana wajibu kulinda vituo hivyo kwa gharama yoyote bila kujali itikadi za kidini na kisiasa.
Wito huo umetolewal eo Oktoba 26,2025 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi Dkt Evaline Munisi ambapo kutokana na amani na mshikamano uliopo Tanzania utulivu huo haupo kwa bahati mbaya unatokana na misingi bora ambayo imekwa na viongozi wetu wa kisiasal
wanaosimamia uchaguzi wenyewe yaani Ofisi ya Msajili wa vyama vya kisiasa tume huru ya Uchaguzi kwani tangu waaanze Kampeni hawajasikia matatizo yeyote.

“Kampeni za awamu hii zimekuwa za tofauti na zile zilizopita sababu zinaenda kidiplomasia na tunashinda kwa hoja kila mmoja akinadi ilani ya Chama chake hatukusikia tena mgombea kwa mgombea wakigombana au kulumbana haya ni matunda na matokeo ya maelezi ya mlezi wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi kongole sana kwake” amesisitiza Dkt Eveline.
Sambamba na hayo amebainisha kuwa bado kuna viashiria ambavyo havina tija kwa Taifa letu kwani kuna baadhi ya watu wanafanya chokochoko na kusababisha taharuki kwa watanzania wanahamasisha kutotii Sheria na kupandikiza chuki ili kuyumbisha Dola hivyo Wananchi msiwasikilize kabisa
Aidha wote wamehamasishwa kuhakikisha Oktoba 29, wanatumia haki Yao ya kikatiba Kupiga Kura


