.

Ndege iliyokuwa na watu 12 imeanguka katika eneo la kaunti ya Kwale, pwani ya Kenya.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KCAA) Emile Arao amethibitisha kwamba ndege hiyo, nambari ya usajili 5Y-CCA, iliyokuwa na watalii ilikuwa ikielekea Kichwa Tembo eneo la Maasai Mara kutoka Diani kabla ya kuanguka.

Picha zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha ndege hiyo ikiwaka moto.

Sababu ya ajali hiyo haikujulikana mara moja na polisi na watoa huduma wengine wa dharura walikimbilia eneo la tukio mara tu baada ya ajali hiyo kutokea.