Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi jijini Dodoma, leo Jumatano, Novemba 5, 2025.
Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimefanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na nafasi ya Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.




