Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Kawaida amewataka wanasiasa kuacha kutumia lugha Mbalimbali ninazoweza kupelekea kuligawa Taifa kufuatia matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea tarehe ya29 na 30 Oktoba 2025, akisema kwa masikitiko kuwa vurugu hizo zimefanywa kwa kiasi kikubwa na vijana kundi analowajibika kuliongoza .

Kawaida amevunja ukimya na kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea na kutoa pole kwa wale wote walipoteza Maisha na waliopata athari za Mali zao kuharibiwa

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam November 9,2025 Mwenyekiti huyo amesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulioipa CCM ushindi mkubwa, lakini umeacha alama ya huzuni kutokana na vitendo vya fujo na uharibifu vilivyotekelezwa na baadhi ya vijana huku wengine kwapoteza ndugu Jamaa naarafiki

“Nimesimama mbele yenu leo si kwa furaha, bali kwa huzuni kubwa. Uchaguzi uliopita ulikuwa ushindi kwa chama chetu, lakini pia ulikuwa somo zito kwa taifa,” amesema Kawaida

Amesema kuwa sehemu kubwa ya vurugu hizo zilichochewa na watu walio wanaotumia mitandao ya kijamii waliwashawishi vijana walio ndani ya Tanzania kufanya vurugu huku wao wakiwa salama na wakifadhiliwa na watu wasioitakia mema nchi. “Ni jambo la kuhuzunisha kuona vijana wenye nia njema wakitumiwa vibaya na watu wanaotaka kuivuruga Tanzania,”

Hata hivyo amebainisha kuwa vitendo hivyo vimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na binafsi, vikiwemo vituo vya polisi, vituo vya mabasi, zahanati, maduka na miundombinu ya barabara na cha kusikitisha zaidi, baadhi ya waliojeruhiwa katika vurugu hizo walishindwa kupata matibabu kwa sababu walikuwa tayari wamechoma zahanati walizotegemea kwa huduma za kwanza,

Mwenyekiti huyo amekemea vikali vurugu hizo, akisema hazikuwa maandamano halali kwa mujibu wa sheria za Tanzania, bali ni vitendo vya uhalifu vilivyoleta hasara kubwa kiuchumi na kijamii. Ameongeza kuwa vurugu hizo ziliathiri biashara nyingi, kuathiri kipato cha wananchi, na hata kuzuia shughuli za bandari zinazohudumia nchi jirani.

“Vijana wenzangu, amani ndiyo msingi wa maendeleo. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya umoja, amani na upendo. Tukicheza na amani, tunacheza na uchumi wetu, na ajira zetu,” amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha amewasisitiza Vijana kutambua kuwa wanapoamka kila.asubuhi wafikirie wale wanaowategemea kupata mahitaji ya Kila siku ikiwemo chakula na mavazi.